Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,234
- 28,473
MAGARI ZAIDI YA 1,500 YASHUSHWA KWA WIKI MOJA BANDARI YA MTWARA,DRC, ZAMBIA NA MALAWI ZANUFAIKA
Bandari ya Mtwara imeendelea kujiimarisha kama lango muhimu la biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuhudumia meli nne ndani ya wiki moja na kushusha zaidi ya magari makubwa 1,500.
Magari hayo yanahudumia soko la Tanzania na kusafirishwa pia kuelekea DRC, Zambia na Malawi kupitia Mtwara Corridor, hatua inayoongeza umuhimu wa bandari hiyo katika mtandao wa biashara wa kikanda.
Mafanikio hayo yanahusishwa na maboresho yanayoendelea kufanywa na TPA, yakiwemo uboreshaji wa miundombinu, matumizi ya teknolojia za kisasa, uwekezaji katika mifumo ya TEHAMA, punguzo la baadhi ya tozo na kuimarishwa kwa ufanisi wa huduma.