Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salama wana JF!Niliuziwa kiwanja mbele ya adv. Kwa kupitia bank, kumbe hakina njia (sala2,DSM)nikatoa adv.20m,muuzaji amenizungusha,sasa sikitaki nataka mwanasheria atakaye recover hy pesa nimpe 2m.
Nawashukuru nyote:Mkuu, 1.mkataba unasemaje?2. Nani aliyeandaa huo mkataba? 3.Je ulikagua hicho kiwanja kabla ya kusaini hati ya makubalino?4. Je, muuzaji alikuwa na wajibu wa kukupatia njia kulingana na makubaliano yenu? 5.Je umenunua kiwanja pamoja na njia au umenunua kiwanja pekee? Mkataba unasemaje?.Ukiyajibu haya maswali basi utaweza kujua umesimama wapi katika madai ya marejesho ya hiyo 20 milioni.
Mzee ulinunuaje mali pasi kutafiti eneo husika?? kurecovery inategemea na masharti ya makubaliano katika Mkataba wenu wa mauzo na iwapo taarifa za hali jhalisi ya kiwanja kulifichwa na kwa ufahamu wako hukuweza kuelewa (misrepresenation).a)Nadhani huyo Adv aliyekusaidia angekuwa mzuri zaidi pia kukueleza sheria na kama kuna tatizo juu ya Makataba wenu ni vyema ungemjulisha shida ilipo ili kama anaweza akusaidie kwa kuzingatia na "facts" kamili ya issue yako.
b)Kwa ushauri tu, kitaaluma, haishauriwi wala kuruhusiwa kwa Mwanasheria kupokea fedha ya Mteja katika suala linalohusu mabishano katika madai au kesi ya Mahakamani (contentious matters) kwa makubaliano kuwa atashinda. Vinginevyo utadanganywa tena. Hakuna Makubalina kama hayo kwani asipoweza ku recover hiyo hela yako, utamdai?? au ikiwa italazimika kufikishana Mahakamani, hiyo 2M itatosha kushughulikia kesi??..
Mwenye eneo(njia) anadai hata kama nikitoa 100M hatoniuzia hiyo njia wala kuniruhusu kuitumia ndio maana naona si vyema nikaishi na majirani wa hivyo. Kesi?unachosema ni kweli na sina subira maana pesa yenyewe nilikopa benki nikijua nimemaliza jambo moja kumbe ndio nimezua balaaa maishani,sasa nakatwa benki kila mwezi.Pole, kanunue eneo uweke njia, ukienda mahakamani ndugu ni soo, kama wewe sio kina Chenge au Marehemu Dito kesi itakaa miaka kibao utafikiri mtoto, mie na kesi ya design hiyo toka 2003 mpaka leo, kwa mwaka inatajwa mara 4 tu kati ya hizo 2 mawakili hawapo, 1 hakimu ana udhuru hiyo 1 ndiyo inasikilizwa na unakuta kuna PO. Yaani unaweza ukafungwa wewe kwa hasira