Natofautiana na wenzangu kuhusu suala la Katiba Mpya

Natofautiana na wenzangu kuhusu suala la Katiba Mpya

Katiba mpya inampunguzia rais madaraka, na bunge litakuwa na madaraka zaidi ya kuwapitisha wateule wa rais. Naogopa asije tokea mwendawazimu akawa rais akamchagua mkewe, wanae, na ukoo wake mzima kwenye madaraka. Mmesahau Iddi Amin alitumia katiba mbovu ya Uganda kujifanyia anavyotaka?
 
Wakati mwingine ninapata wasiwasi na baadhi ya wanajamvi ni kama vile wana ajenda zao za siri,hili la sokomoko nalifananisha na lile la takukuru kujifanya inaleta mjadala wa kuwaoji wabunge kuhusu kupokea posho mara mbili,wakati mambo ya richmond yaeiva yako jikoni(bungeni) yanajadiliwa baada ya ripoti ya mwakemye,hii ilikuwa ni mbiunu chafu ya ccm na serikali kuwanyamazisha wabunge na kubadilisha muelekeo ili kutuliza mkasa wa richmondology,huyu mwenzetu ni kama ana lake jambo hatujamaliza hili la msingi ambalo liko mbeleyetu anataka kuleta danganya toto,hatudanganyiki tumekushtukia una lako jambo,kama unania ya kweli anza moja kisha mbili na sio moja na mbili kwa pamoja kwani yawezakukuponyoka yote mawili...............
 
Habari zenu wanaJF,

Napenda nitofautiane kidogo na wenzangu kuhusu hili suala la Katiba mpya. Kwangu mimi kipaumbele cha kwanza ni mishahara mikubwa na posho nono wanazopewa wabunge. Kama kweli wabunge wetu ni wazalendo wangeanza na hili na kuhakikisha kabla ya bunge la bajeti 2011/2012 limefanikiwa na kinachobakia kwenye mishahara ikaenda kuongezewa kwa waalimu na wauguzi. Maana watu watakuwa busy kwa miaka mitano kudai katiba mpya huku watoto wetu wakipewa elimu mbovu na huduma mbaya za afya kwakuwa wauguzi na waalimu maslahi yao yamemezwa na waheshimiwa wabunge!

Halafu mwaka 2011 baada ya kikao cha bajeti waanze mchakato wa katiba mpya sambamba na kubadilisha katiba zao za vyama maana hata huko kwenye vyama katiba hazikidhi matakwa ya wengi. Sipendi kutolea mifano ila ipo mingi sana kwenye baadhi ya vyama vyetu kuna uditekta, kujuana na undugu.

Nawakilisha....

Ishi...! Hujui au unajifanya maamuma, Katiba Ya Nchi ndo SHERIA MAMA na sheria zote zinatoka humo! Ukitaka kuangamiza mti, ng'oa mzizi wake mkuu siyo unachuma majani au matunda?

Umesahau kuweka ufamilia kwenye red! Maana hapa unawalenga CC-M!
 
Back
Top Bottom