Natokwa na maji machafu kwenye kucha za miguu, naomba kujuzwa tiba yake

Natokwa na maji machafu kwenye kucha za miguu, naomba kujuzwa tiba yake

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ndugu zangu natokwa na maji kwenye kucha za miguu alafu kucha zenyewe zinaonesha dalili za kuharibika tatizo ni nini? na nini tiba yake?

1591104565221.png
 
Yaweza kuwa ni fungus

Pia wagonjwa wa kisukari pia Huandamwa sana na infection Kwenye kucha za vidole

Iko haja ya kwenda hospital unaweza kupoteza kucha mkuuu
 
Yaweza kuwa ni fungus

Pia wagonjwa wa kisukari pia Huandamwa sana na infection Kwenye kucha za vidole

Iko haja ya kwenda hospital unaweza kupoteza kucha mkuuu
sawa ,kwa hiyo haiusiani na kansa kabisa?
 
mkuu mbona vidole vichafu huogagi wewe? btw nenda hospitali inaweza kuwa fungus au laa
 
sawa ,kwa hiyo haiusiani na kansa kabisa?
Binafsi naweza kusema ni fungal infection

Majibu sahihi utayapata hospital Mkuuu ningeshauri dawa za kutumia lakin si njia bora

Njia sahihi kuhudhuria hospital kisha ukaandikiwa dozi stahiki
 
Binafsi naweza kusema ni fungal infection

Majibu sahihi utayapata hospital Mkuuu ningeshauri dawa za kutumia lakin si njia bora

Njia sahihi kuhudhuria hospital kisha ukaandikiwa dozi stahiki
sawa mkuu nashukuru
 
Huenda ikawa ni growing nail problem...hii hutokana na mwili kuongezeka uzito na size ....hasa kama huna mazoea ya kukata kucha halafu unavaa viatu mda mwingi...hii hufanya nyama kuziba njia ya kucha hivyo kujikuta kucha zikichimba ktk kuta za vidole hasa dole kubwa...hivi vidonda huwa si sana rahisi kupona...husababisha usaha...majimaji na wkt mwngne damu pia...

Mimi nilipatwa na hili tatizo mwezi mei niliteseka mwezi mzima....lkn nilienda dispensary moja IPO pale kigogo mwisho nikafanyiwa operation ndogo kwa kung' oa sehemu ya ukucha iliyoathirika ili kuruhusu kidonda kupona ikiwa umeathirika zaidi ukucha mzima unaweza kutolewa na hata ukiota huwa dhaifu...gharama yake ni tsh. 20,000 kwa kidole kimoja pamoja na dawa...Ila utangolewa kwa interval ya siku mbili...maana changamoto kidogo...Mungu akutie nguvu mkuu utapona
 
Back
Top Bottom