Natokwa na mvi kwenye ndevu bado mdogo

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Hi Jf doctors
Nimeshtuka juzi hapa naona mvi 3 kwenye ndevu wakati ndevu zenyewe za mawazo.
Nimeuliza watu wanasema eti na dalaili ya kua na hela mingiii.
Haziwezi kuwa nyingi kidevuni?
Hazina madhara?
Nifanyaje zitoke na zisirud?
Umri 20-27
 
Umri umesogea mzee.. Pesa na ndevu nyeupe wapi na wapi? Kwani kuwa na mvi ni kumiliki kiwanda cha kutengeneza pesa?
Kwakweli nami nashangaa watu imani zao..
Bado mkuu umri haujafika mbali niko early 20
 
Mara nyingi ulaji wa karoti kwa wingi huondoa tatizo la kuota mvi mapema.

Ndio maana Wachina wanasifika kwa kutokuwa na mvi za haraka japo wanakuwa wazee kwa sababu ya kula karoti kwa wingi.

Sijajua kwa ndevu inakuwaje, kama ni mvi za kawaida kama za kichwani, ila mara nyingi kuna mvi za urithi(za ukoo), ambazo zinatokana na genetics tu.

Jaribu kuchunguza ukoo wenu hususani mababa na wajomba, kama wanazo hasa kwenye ndevu basi zitakuwa za ukoo hizo ambazo hazinaga dawa zaidi ya kuzinyoa.

Lakini kama ni za kawaida basi tumia karoti kwa wingi.
 
Ahsante sana kwa ushauri mkuu. Kwetu hakuna mvi ki ivo hata mzee hana..
 
Ahsante sana kwa ushauri mkuu. Kwetu hakuna mvi ki ivo hata mzee hana..
Cheki pia ukoo wa mama, maana huko nako huwa kuna kuchukua vinasaba.

Kumbuka mvi za ndevu zina tofauti sana na mvi za kichwani, wengi wenye mvi za idevuni huwa hawana mvi za kichwani.
 
Huo ndio mwanzo wa kukaribia zone ya uhenga. Be proud of it mzee baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…