Natokwa na usaha sehemu za siri!

Japhet92

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2015
Posts
209
Reaction score
312
Poleni na Majukumu.

Miezi 2 iliyopita nilikutana kimwili na demu wangu wa siku nyingi ambaye tulikuwa hatujaonana takribani miaka 3. Hatukutumia kinga. Baada ya wiki 1 nikaanza kutokwa usaha sehemu za siri. NIlipoenda kupima nkaambiwa nina U.T.I na nikapewa Norfloxin. Nilimaliza dozi lakini tatizo liliendelea.

Nikabadilishiwa dawa na kupewa Augumentin lakini nayo iligonga mwamba. Nkapewa Flumox lakini kila nilipopima wadudu walionekana kupungua lakini hawakuisha mwilini.

Daktari akanishauri nikapime Urine for culture and sensitivity ambapo niliambiwa siumwi magonjwa ya zinaa. Majibu yaliandikwa "yielded a heavy growth of longue storplycoca" na kushauriwa kuwa nitumie dawa mojawapo kati ya Chloramphenicol, Gentamicyin au Tetracycline ntapoina lakini mpaka sasa nimeshatumikia dawa mbili kati ya hizo lakini bado natokwa na majimaji yanayoteleza na yenye harufu mbaya.

Naombeni msaada hawa ni wadudu gani sugu kiasi hiki? Kama kuna ambae amewahi kuumwa kama mimi ulipona kwa dawa gani?

Nisaidieni mwenzenu maana kuna wakati hao wadudu wakichachamaa nasikia maumivu makali sana ya uume.

Yeyote anayewafahamu hawa wadudu nisaidieni the way to overcome this.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Duuuuh poleeee.wataalam wanakujaa😯😯😯😯
 
pole ila ndo mkome kuhangaika c mnadai kugonga ovyo ndo udume.
but tafuta wataalam zaid watakusaidia ikiwezekana kapme kwa mara nyingne
 
Kingine angalia dawa zako unanunua wapi, pharmacy zingine wanauza fake au zilizoexpire na inawezekana ndio maana hauponi.
 
Hiyo condtion mbona ni dalili halisi za std na hata hizo dawa za round ya pili ni za std. Unapaswa upate mtaalam abaini ni std gani na imeshakuwa chronic kwa kiasi gani. Bila kubaini hivyo, unaweza ukaendelea kuteseka kwa mda mrefu na kupata madhara zaidi
 
Pole sana,hope ulienda kwenye vihosptal vidogo hiv binafsi..nenda hospital kubwa kwa vipimo zaid hiv vi dspensary mara nying hakuna wataalam wa kutosha..wahi hospital ya wilaya au mkoa fanya haraka hayo magonjwa yakikomaa hupelekea ugumba so wahi kabla tatizo halijazaa tatizo lingine kubwa zaid.
 
nenda hospital kubwa mkuu pole sana tena sana,lakin pia nakushauri usiwe na aibu na hayo mambo jitose hospital ongea na doctor kinagaubaga na ukipima urudie kupima na kwingine.
 
Japhet najua lazima utakuwa umepima syphilis. Kama bado kacheck. Japo sijui mtu alipata syphilis huwa inajionyesha baada ya mda gani.

Kama kweli una UTI. Basi itakuwa labda imeingia kwenye korodani zako.

Nashauri uende kwa daktari wa ngozi. Hawa ndo madaktari wa magonjwa ya zinaa.

Dawa moja nzuri sana ya UTI iliyokomaa ni LOMEFLOXACIN. Ila inabidi utumie kwa mwezi mzima. Kila siku kidonge kimoja ikiwezekana ucku ili usipate adhari za jua.
 
Wakati tunasuburia wataalam waje kutoa majibu, tangu ulipopata hilo tatizo unaendelea kufanya tendo la ndoa? Kama jibu ni ndio, unafanya na mtu mmoja au wengi na hao hali zao zikoje? Usije kua unajitibu wewe kumbe mwenzio/wenzio wana hali mbaya na kila unapoenda unaongezea matatizo mkuu.
 
Duuh pole wa jina Mungu akusudie upone! Ila siku nyingne wajina tumia kinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…