Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
usawa huu hutumii kinga loh
Poleni na Majukumu.
Miezi 2 iliyopita nilikutana kimwili na demu wangu wa siku nyingi ambaye tulikuwa hatujaonana takribani miaka 3. Hatukutumia kinga. Baada ya wiki 1 nikaanza kutokwa usaha sehemu za siri. NIlipoenda kupima nkaambiwa nina U.T.I na nikapewa Norfloxin. Nilimaliza dozi lakini tatizo liliendelea.
Nikabadilishiwa dawa na kupewa Augumentin lakini nayo iligonga mwamba. Nkapewa Flumox lakini kila nilipopima wadudu walionekana kupungua lakini hawakuisha mwilini.
Daktari akanishauri nikapime Urine for culture and sensitivity ambapo niliambiwa siumwi magonjwa ya zinaa. Majibu yaliandikwa "yielded a heavy growth of longue storplycoca" na kushauriwa kuwa nitumie dawa mojawapo kati ya Chloramphenicol, Gentamicyin au Tetracycline ntapoina lakini mpaka sasa nimeshatumikia dawa mbili kati ya hizo lakini bado natokwa na majimaji yanayoteleza na yenye harufu mbaya.
Naombeni msaada hawa ni wadudu gani sugu kiasi hiki? Kama kuna ambae amewahi kuumwa kama mimi ulipona kwa dawa gani?
Nisaidieni mwenzenu maana kuna wakati hao wadudu wakichachamaa nasikia maumivu makali sana ya uume.
Yeyote anayewafahamu hawa wadudu nisaidieni the way to overcome this.
Natanguliza shukrani zangu.