jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Amekutapeli nini??kwanini hammpeleki mahakamani kama ni tapeli??Acha kukufuru, unamlinganisha tapeli Mwamposa na yesu.Mwamposa atapata heshima akijikita kwenye kuhubiri, lakini figisu za kutayarisha watu wazima na kuwapa magongo ili watoe ushuhuda wa uongo ajue ni dhambi. HANA TOFAUTI NA MATAPELI YA KALYNDA. Anajishushia heshima.
Wengi mnao mponda mwamposa ni wachungaji uchwara mnaona waumini wanawakimbia mmeanza kukosa sadaka sasa kilichobaki ni kuanzisha bifu na chuki dhidi ya mwamposa kama yule shehe ubwabwa wa dsm.Sijaona mtu wa Mungu ana mitusi kama wewe. Nilifikri utageuza shavu la pili, kumbe tukikuambia Mwamposa ni tapeli unakasirika. Basi usingeleta hii mada huku. Usijekutuiambukiza ujinga na sisi tukakubali kutapeliwa. Hata wale wa Kalynda walitumwa kuaminisha watu ule utapeli ilikuwa ukombozi wa umaskini. Kama Mwamposa anazo hizo nguvu, kwa nini analilia sadaka. Si amuombe amshushie $ na Euro kuliko kuwanyang'anya maskini kile kidogo walichonacho kwa kuwadanganya Mungu atawarudishia mara saba! Tapeli na mwizi wa imani huyo nabii wako.
Kama kupotea kila mtu atapotea hao manabii na mitume wote walishapotea kila kiumbe duniani kitapotea hilo sio geni.time will tell kwani gwaji boy yuko wapi si alianza hivi hivi. hawa manabii uchwara ni moto wa kifuu baada ya mda wanapotea km hawakuwepo maana ubaya ukifanya vitu bila nguvu za Roho mtakatifu kuna mwisho wake tu.
note. huwezi ukadanganya watu wote kwa wakati wote
Ila nayehubiriwa ni nani..?au yeye mwamposa ana biblia yake kutoka mbeya..??bandiko la post limelenga kumuinua mwamposa ila si kumtukuza Mungu si shangai ndo maana hakuna sehemu ametajwa Mungu wala Yesu hata kwny matangazo mengine unakuta anasifiwa yeye tu.
Mungu akimuita mtu kuwa nabii ni lazima utukufu apewe Mungu. ila ukiona utukufu hapewi Mungu unajua kwa huyo nabii Mungu hayupo
Uponyaji wa kiimani haupo hivyo..yani kila sehemu wewe ni kuombea watu tu wenye shida..hata Yesu hakufanya hivyo..bali wenyeshida ndio waliokuja kwake na yeye aliwaponya na kisha kuwaambia imani yako imekuponya..first imani itoke kwa muhitaji wa uponyaji ndio uponyaji utatenda kazi.Yule mdada WAKONTA MAPUNDA kila siku wanampita kama hawamuoni, Namuomba mwamposa aende kumuombea yule dada kwa jina la yesu.
Basi kaa utulie kama huna hoja ya msingi..baki na imani yako.Mkuu hilo ni swala la imani so hata kama nikikupa sababu mia bado huwezi nielewa kwani imani yako iko kwake kama ambavyo imani yangu haiko kwake
Kama alitengeneza siku za karibuni kuna ubaya..hivi mbona una akili ndogo hivi..kwahiyo ulitaka maisha yake yote awe na gongo la miaka 15 ilo pita..kwamba magongo haya chakai na kuharibika.?Kuna mzee leo kajitokeza kutoa usuhuda kuwa alikuwa hawezi kutembea kwa miaka 15 anatembelea gongo lakini mamposa kamponya ila cha ajabu gongo lake naye ni jipya
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tuelekeze pia mahali ambapo watu walikanyagana mpaka wakafa kwa kutafuta huduma yake.Hata Bwana wetu Yesu hakuponya wote aisee.
Hapa ndipo huwa nashangaa watu,eti mtu humjui Wala nini,anashuhudia kapona na wewe unaamini!akijibu na yeye ni kilema unitag
Faith healing haifanyi kazi hivyo..hata Yesu hakuenda hospitali bali walimfuata alipo ili awaponye na mwisho wasiku aliwaambia imani yako imekuponya.Nashangaa mtu anaeamini yale maigizo,,
Wagonjwa wamejaa mahospitali wanapumulia mipira,
Wagonjwa wa kansa wamejaa ocean road,
Wenye matatizo ya moyo wamejaa taasisi ya JK
Vichaa wamejaa mirembe,
Wagonjwa wa figo wapo muhimbili,
Kwanini huyo mwamposa asinde kuwaponya hao wagonjwa wanateseka na hawajui hatma yao??
Mtu anafunga safari kutoka Mtwara mpaka Songea na anarudi kama alivyokwenda.Ukiona hivyo hawana imani..halafu faith healing haiendi mnavyotaka nyie..lazima ianzie moyoni kwa mhuhusika yana yule anayehitaji uponyaji..tusema mara ngapi muelewe.
Imani kwanza ndio itakayokupa uponyaji.
#MaendeleoHayanaChama