Natural death ni uzee na kuugua tu vifo vingine tumevitengeneza binadamu

Natural death ni uzee na kuugua tu vifo vingine tumevitengeneza binadamu

Wakuu habari zenu Leo Niko hapa kuongelea kuhusu natural death

VIFO ambavyo binadamu tulipaswa tufe ni kutokana na kuuzeeka au magonjwa

Ila aina zingine za Vifo zinaletwa na ujuaji wetu Ujanja Ujanja wa ku innovate vitu Kwa kusingizia maendeleo ya science and technology

Assume Dunia bila gari Wala chanzo chochote Cha usafiri kisingekuwepo Kuna ambae angekufa Kwa ajari?

Na aina zingine mbali mbali za Vifo vyote tumevitengeneza binadamu wenyewe
Tungekufa tu hata kwa kuangushwa na farasi
 
Hivyo vimbunga tumsingizie Mungu na ndugu yake shetan wao ndio wasababishaji wa hizo natural disasters.

Na hii iwaendee wale wanaosema kifo cha fulani sijui ni Mungu kapanga ama sijui shetan kasababisha, huu ni uzushi, Vifo vingi kwa sasa hasa ajali ni uzembe wa watu kutofuata taratibu&sheria, pili baadhi ya majanga hasa mafuliko yanapoua raia hapo ni uzembe wa raia kuweka makazi ktk maeneo hatarishi haswa kujenga kwenye mikondo ya maji.

Hata huko mahospitalin ndiko hovyo kabisa, wagonjwa hawatibiwi kwa viwango vinavyohitajika, wengi wao wanakufa kwa uzembe wa wauguzi wetu ama uzembe wa raia kutofika hospitali kwa wakati ama uzembe wa serikali kutokidhi miundombinu ya usafirishaji ama uwepo&ubora wa vifaa tiba mahospitali.

Kiufupi ni kwamba, jinsi tunavyofanikiwa kitechnolojia ndivyo hata kifo tunakisogelea badala ya kukiepuka.

Uzembe kila mahala,
Kuhusu majanga ya asili, Mungu wala shetani hawahusiki ila ni shunguli za kibinadamu ndio sababu
 
Back
Top Bottom