Nature preserved! Only for nature lovers

Nature preserved! Only for nature lovers

FB_IMG_1647742148200.jpg
 
Wapendwa,

Kama mtakuwa mmenotisi, hivi Karibuni joto wakati wa mchana na usiku limekuwa juu sana [emoji30] [emoji29] Hii ni kutokana na mawimbi ya joto yanayotokana na utoaji wa gesi chafuzi Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Afrika Mashariki imewatahadharisha watu kujiandaa kwa siku zijazo za joto na usiku wenye joto.

Maandalizi haya yatahitaji mikakati mahiri ya kukabiliana na hali ya hewa na kujihusisha katika mazoea ya kustahimili hali ya hewa. ili kukabiliana na uharibifu ambao umefanywa.

Madhara ya kawaida ya mawimbi ya joto kwa binadamu ni upungufu wa maji mwilini ambao unaweza kusababisha kuzirai au kifo, tetekuwanga, vipele vya joto, na msongo wa mawazo. Ili kukabiliana na hali ya hewa ya sasa, wataalamu wameshauri kuwa;
Inapaswa kunywa maji zaidi ili kuweka maji mwilini. Kuwa na chupa yako ya maji pembeni ili kukukumbusha kunywa kila wakati. Epuka vinywaji vyenye kileo na kafeini katika kipindi hiki. Punguza ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi kwa sababu huongeza joto la kimetaboliki. Vyakula safi, matunda na mboga ni chaguo bora zaidi.

Fuatilia shinikizo la damu yako, iwezekanavyo, Kaa ndani ya nyumba majira ya mchana 6:00 na 9:00 alasiri. Unapaswa kuoga maji baridi kwa kumwaga maji kwanza kwenye miguu yako pole pole kueelekea juu, na hatimae kichwani, ili kuzuia uwezekano wa kupatwa na kiharusi (stroke) au kifo. Fanya hivyo kila siku kabla ya kulala usiku.

Tafadhali jitahidi kuzingatia, Bado tunakuhitaji ukiwa mwenye afya tele![emoji177]
 
Back
Top Bottom