Nauachaje huu mchepuko?

Nauachaje huu mchepuko?

Mbwa mpumbavu katika moja na mbili,
1000012539.jpg
 
Mm kama mwanaume mwenzio nakushauri tu km kweli umemchokaa mpe hata Mali kdg kuliko kumnyima kabisaa na umwambie ukweli kuwa umuhitaji Tena japo ataumia lkn ndio hvyo ...

Ila nyegeee mmmhhh...
 
😅😅😅😅 hakikaa na achapwe viboko..
 
Mimi ni Baba wa watoto watatu, nimeoa ndoa yenye miaka 12 sasa. Kuna sehemu niko nafanya kazi mke wangu naye ni mfanyakazi na ni ngumu kuhama basi tunahisi tofauti.

Hapa ofisini kuna dada nimeanza naye mahusiano ni mwaka 4 sasa, ni kama nimehamia kwake nilipokuwa nimepanga mimi naweza kukaa hata miezi 6 siendi huko, kila mtu anafahamu kuwa huyu ni mke wangu hata ofisini kila kitu tunafanya pamoja wanajua nishaachana na mke wangu.

Wakati nakutana naye nilimuambia kuwa nimeoa na kipindi hicho mke wangu alikua anakuja huku bila shida ila baadaye nilimkataza kwakua ndiyo mimi naenda tu.

Kashanitambulisha kwao na mimi kwetu kuna baadhi ya ndugu wanamfahamu. Anaamini nitamuoa na kweli kuna kipindi mimi na mke wangu mahusiano yaliyumba tukaenda mpaka mahakamani kufuatilia talaka lakini mke aligoma hivyo niliacha mambo ya kufuatilia.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, nimemchoka huyu dada na kweli sasa hivi nataka kurudi kwenye ndoa yangu. Naona kama nampotezea mdua ana miaka 33 hana mahusiano mengine ni kama anasubiria mimi kauchana na mke wangu, naona ashaanza kisirani ananichunga kama mke kitu amabcho sitaki!

Shida inakuja kwamba kuna vitu vingi vya maendeleo nimefanya naye, tumejenga nyumba mbili, tuna gari na biashara ambayo kila kitu kina majina yangu lakini yeye alichangia kwani alichukua mpaka mikopo akiamini mimi ni mume wake kwakua tu sina mawasiliano mazuri na mke wangu.

Hofu yangu ni kwamba nikitaka kumuacha atadai mali kitu ambacho siko tayari kumpa. Kuna watu wananishauri kubadilisha hizi mali kuandika majina ya wanangu, nauliza je ana haki yoyote.

Mimi nayeye hatuna mtoto nimekua makini sana kuhakikisha simpi mimba ila yeye ana mtoto alizaa na mwanaume mwingine na tunaishi naye, nimechoka nataka kurudi kwenye familia yangu, je namuondoaje huyu Bibie bila kumpa chochote.

Nimejaribu kuhangaika ili ahamishwe mkoa lakini imekua ngumu, kila nikihangaika anabana. Kwakweli nimechoka haya maisha ya kuishi na mchepuko, nataka kwenda kumchukua mke wangu tuishi pamoja kwani huu umbali mke wangu naye asije kuchepuka, nisaidie nafanya nini?
Kwahiyo unataka umuachie maumivu mara mbili huyo mwanadada? Mpe nyumba moja na gari wewe rudi kwa mkeo hapo angalau hatokulaani sana... umejitahidi kwenye swala la mimba ila umefeli kwenye uwekezaji.
 
chai zako unapika vizuri kweli 🤓 cheki kama hiyo .
 
Nawaza tu maumivu atakayoyapata atapogundua amepoteza Mda kuwekeza muda, Mali na hisia mahali pasipo sahihi
Sometimes wanaume tunazingua sana aisee, afu utamkuta mtoa mada anapinga mwanaume mwngn kuoa single maza
 
Vithread vya namna hii vinatoa watu sumu mwilini, ni kama kumgusa cobra mkia, lazima akutemee sumu.

Episode nyingine ya mzee wa hovyo🤣🤣🤣

CC: Atoto
 
Mkeo huyu huyu mama jamila anaetembea na bosco mwenye duka la dawa mwaka wa pili huu na ana mimba ya kujifungua? Pole zakaria
 
Mimi ni Baba wa watoto watatu, nimeoa ndoa yenye miaka 12 sasa. Kuna sehemu niko nafanya kazi mke wangu naye ni mfanyakazi na ni ngumu kuhama basi tunahisi tofauti.

Hapa ofisini kuna dada nimeanza naye mahusiano ni mwaka 4 sasa, ni kama nimehamia kwake nilipokuwa nimepanga mimi naweza kukaa hata miezi 6 siendi huko, kila mtu anafahamu kuwa huyu ni mke wangu hata ofisini kila kitu tunafanya pamoja wanajua nishaachana na mke wangu.

Wakati nakutana naye nilimuambia kuwa nimeoa na kipindi hicho mke wangu alikua anakuja huku bila shida ila baadaye nilimkataza kwakua ndiyo mimi naenda tu.

Kashanitambulisha kwao na mimi kwetu kuna baadhi ya ndugu wanamfahamu. Anaamini nitamuoa na kweli kuna kipindi mimi na mke wangu mahusiano yaliyumba tukaenda mpaka mahakamani kufuatilia talaka lakini mke aligoma hivyo niliacha mambo ya kufuatilia.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, nimemchoka huyu dada na kweli sasa hivi nataka kurudi kwenye ndoa yangu. Naona kama nampotezea mdua ana miaka 33 hana mahusiano mengine ni kama anasubiria mimi kauchana na mke wangu, naona ashaanza kisirani ananichunga kama mke kitu amabcho sitaki!

Shida inakuja kwamba kuna vitu vingi vya maendeleo nimefanya naye, tumejenga nyumba mbili, tuna gari na biashara ambayo kila kitu kina majina yangu lakini yeye alichangia kwani alichukua mpaka mikopo akiamini mimi ni mume wake kwakua tu sina mawasiliano mazuri na mke wangu.

Hofu yangu ni kwamba nikitaka kumuacha atadai mali kitu ambacho siko tayari kumpa. Kuna watu wananishauri kubadilisha hizi mali kuandika majina ya wanangu, nauliza je ana haki yoyote.

Mimi nayeye hatuna mtoto nimekua makini sana kuhakikisha simpi mimba ila yeye ana mtoto alizaa na mwanaume mwingine na tunaishi naye, nimechoka nataka kurudi kwenye familia yangu, je namuondoaje huyu Bibie bila kumpa chochote.

Nimejaribu kuhangaika ili ahamishwe mkoa lakini imekua ngumu, kila nikihangaika anabana. Kwakweli nimechoka haya maisha ya kuishi na mchepuko, nataka kwenda kumchukua mke wangu tuishi pamoja kwani huu umbali mke wangu naye asije kuchepuka, nisaidie nafanya nini?
IMG_20240824_215431.jpg

Mbaga Jr
 
Kwani huko kwenu hawaruhusu mke mdogo Sheikh??
 
Back
Top Bottom