KWELI Nauli kwenda mikoani zapanda kuanzia Mei, 2022

KWELI Nauli kwenda mikoani zapanda kuanzia Mei, 2022

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wasafiri wa maeneo mbalimbali wameripoti nauli za mabasi kwenda mikoani kupanda.

1657980374762.png
 
Tunachokijua
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ni Mamlaka ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 3 ya mwaka 2019. Sheria hii ilifuta Sheria ya iliyokuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

LATRA imepewa jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri ardhini, hususan usafiri wa mizigo na abiria (mabasa ya njia ndefu, mabasi ya mijini, magari ya mizigo, teksi, pikipiki za magurumu mawili na matatu) usafiri wa reli na usafiri wa waya.

Ni kweli kuwa nauli zimepanda?
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imethibitisha kutangaza nauli mpya za mabasi ya masafa marefu tar Aprili 30, 2022.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.

nauli-jpeg.2206035
Mpangilio wa nauli mpya utakaoanza kutumika kuanzia Mei 1, 2022.
Huu ni uthibitisho wa andiko la Mdau wa JamiiForums alilochapisha Aprili 20, 2022 likiwa na kichwa cha habari Nauli kwenda mikoani hatimae zapanda. Mama anaupiga mwingi

Hivyo, JamiiForums inathibitisha kuwa gharama ya Nauli imepanda na ilianza kutumika kuanzia Mei 1, 2022.
Back
Top Bottom