Nauli zimeshapanda Arusha licha ya LATRA kupiga marufuku wasafirishaji kupandisha nauli, wananchi watoa milio

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Wimbi la kupanda kwa bei ya mafuta nchini limeanza kuleta mtafaruku mkubwa katika sekta ya usafiri, huku kukiwa na malalamiko mazito kutoka kwa abiria kuhusu ongezeko la nauli kinyume cha sheria.

Malalamiko ya Wananchi
Abiria mmoja mkoani Arusha ameeleza kuwa amekumbana na hali ngumu ya usafiri ambapo nauli zimepanda kutoka Sh. 900 hadi kufikia Sh. 1,500 kwa rura fulani.

"Hali ya usafiri leo ni shida sana. Kutoka sehemu tuliyokuwa tukilipa mia tisa, sasa hivi wanadai elfu na mia tano. Wanadai mafuta yamepanda bei hadi elfu nne kwa lita," alieleza mmoja wa abiria aliyehojiwa na Ayo TV.

Kijana mmoja anayejitambulisha kama mwendesha bodaboda kwa jina la Arone Bryson Yohana, ameelezea kwa masikitiko jinsi kupanda kwa bei ya mafuta kulivyomuwacha kwenye wakati mgumu kuanzia asubuhi.

"Leo yaani nimeamka saa kumi na mbili kwenda sheli (kituo cha mafuta), namwambia niwekee mafuta ya elfu thelathini hapo lita kumi, ananiambia mafuta yamepanda bei, ni elfu arobaini lita kumi. Nikamwambia kwa nini? Ananiambia lita ni elfu tatu na mia tisa na hiyo...

Tukamwambia 'bwana inakuwaje sasa?' Tutateseka, abiria wetu bwana tunaowazolesha bei ya kawaida itakuwaje? Wakasema ndio hivyo mafuta yamepanda bei kutokana na mipaka huko staili gani, kwa hiyo imeshindikana.

Pia soma: Hapa Morogoro kuna baadhi ya maeneo bei ya nauli ya bajaji imepanda mara 2 na maeneo mengine kwa nusu bei
 
Nauli kupanda ni laZima
Tuwafikirie na wamiliki wa vyombo vya moto
 
Wakuu,

Wimbi la kupanda kwa bei ya mafuta nchini limeanza kuleta mtafaruku mkubwa katika sekta ya usafiri, huku kukiwa na malalamiko mazito kutoka kwa abiria kuhusu ongezeko la nauli kinyume cha sheria.

Malalamiko ya Wananchi
Abiria mmoja mkoani Arusha ameeleza kuwa amekumbana na hali ngumu ya usafiri ambapo nauli zimepanda kutoka Sh. 900 hadi kufikia Sh. 1,500 kwa rura fulani.

"Hali ya usafiri leo ni shida sana. Kutoka sehemu tuliyokuwa tukilipa mia tisa, sasa hivi wanadai elfu na mia tano. Wanadai mafuta yamepanda bei hadi elfu nne kwa lita," alieleza mmoja wa abiria aliyehojiwa na Ayo TV.

Kijana mmoja anayejitambulisha kama mwendesha bodaboda kwa jina la Arone Bryson Yohana, ameelezea kwa masikitiko jinsi kupanda kwa bei ya mafuta kulivyomuwacha kwenye wakati mgumu kuanzia asubuhi.

"Leo yaani nimeamka saa kumi na mbili kwenda sheli (kituo cha mafuta), namwambia niwekee mafuta ya elfu thelathini hapo lita kumi, ananiambia mafuta yamepanda bei, ni elfu arobaini lita kumi. Nikamwambia kwa nini? Ananiambia lita ni elfu tatu na mia tisa na hiyo...

Tukamwambia 'bwana inakuwaje sasa?' Tutateseka, abiria wetu bwana tunaowazolesha bei ya kawaida itakuwaje? Wakasema ndio hivyo mafuta yamepanda bei kutokana na mipaka huko staili gani, kwa hiyo imeshindikana.

Yaani nauli kutoka Tsh 900 Hadi 1500?

Naunga mkono sasa CCM kuondoka madarakani kwa 100%
Hii Nchi biashara ya mafuta asilimia kubwa inafanywa na viongozi wakuu, viongozi hawana huruma kabisa na wananchi wao! Yaan nauli inapandishwa kiolela kwa hundred percent,na siku mafuta yakishula hutosikia wakiwatetea wananchi kuwa nauli ipungue
 
Mafuta si yamepanda
Lazima wenye vyombo vya moto wapandishe nao
Kama unaona kadhiaaa piga mguu tu

Ova
 
Nikumaanisha hapa dar mpaka chuga inawezaikafik elfu 70
 
Mafuta yapande halafu Latra imepiga marufuku nauli zisipande.

Hizo ni akili au shahawa?
 
Wanasiasa wapo kimya wanawaza namna ya kucheza na hiyo fursa
 
Back
Top Bottom