Wakuu,
Wimbi la kupanda kwa bei ya mafuta nchini limeanza kuleta mtafaruku mkubwa katika sekta ya usafiri, huku kukiwa na malalamiko mazito kutoka kwa abiria kuhusu ongezeko la nauli kinyume cha sheria.
Malalamiko ya Wananchi
Abiria mmoja mkoani Arusha ameeleza kuwa amekumbana na hali ngumu ya usafiri ambapo nauli zimepanda kutoka Sh. 900 hadi kufikia Sh. 1,500 kwa rura fulani.
"Hali ya usafiri leo ni shida sana. Kutoka sehemu tuliyokuwa tukilipa mia tisa, sasa hivi wanadai elfu na mia tano. Wanadai mafuta yamepanda bei hadi elfu nne kwa lita," alieleza mmoja wa abiria aliyehojiwa na Ayo TV.
Kijana mmoja anayejitambulisha kama mwendesha bodaboda kwa jina la Arone Bryson Yohana, ameelezea kwa masikitiko jinsi kupanda kwa bei ya mafuta kulivyomuwacha kwenye wakati mgumu kuanzia asubuhi.
"Leo yaani nimeamka saa kumi na mbili kwenda sheli (kituo cha mafuta), namwambia niwekee mafuta ya elfu thelathini hapo lita kumi, ananiambia mafuta yamepanda bei, ni elfu arobaini lita kumi. Nikamwambia kwa nini? Ananiambia lita ni elfu tatu na mia tisa na hiyo...
Tukamwambia 'bwana inakuwaje sasa?' Tutateseka, abiria wetu bwana tunaowazolesha bei ya kawaida itakuwaje? Wakasema ndio hivyo mafuta yamepanda bei kutokana na mipaka huko staili gani, kwa hiyo imeshindikana.