Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hana ubavu wa kujibu hiliWakuulizwa hayupo ameshaendazake wengine utawaonea bure!
Labda Mwigulu atakujibu maana hata data za Covid kufichwa alizitetea mpaka akarudishiwa uwaziri
10% ilikuwa ukichelewa kuanza kulipa. Kwamba ukichelewesha marejesho ukizidi kipindi cha neema ndio unapigwa 10% kama faini.Naombeni msaada kwenye mchanganuo wa tozo ya 6% na 10% iliyokua inatozwa na bodi ya mikopo ambayo Mheshimiwa rais alizisamehe siku ya may mosi. Nataka kujua utofaut wake upoje na zilkua zinatozwaje?
Kila mwaka deni lilikua linaongezeka?10% ilikuwa ikichelewa kuanza kulipa. Kwamba ukichelewesha marejesho ukizidi kipindi cha neema ndio unapigwa 10% kama faini.
6% ni value retention fee ambayo ilikuwa ikitozwa kwa outstanding loan kila baada ya mwaka.
Ninachokijua ni kwamba 10% ni pale ambapo ulikuwa unachelewa kutoa taarifa ya kuanza kukatwa mkopo,mfano sheria ya bord inasema ukipata kazi unatakiwa ukae miaka 2 ndoo uanze kukatwa na wakati mwingne hiyo sheria walikuwa hawaifuati,ukimaliza chuo na ukapata kazi haraka sana wanaanza kukata .Sasa Sasa kulingana na hiyo sheria ya miaka miwili ikipita haijarishi una kazi au hauna kazi wanaanza kuongeza asilimia 10% kwenye mkopo wako kila mwaka unaochelewa kulipa na ndoo maana mnufaika alikuwa anaweza kulipa mkopo mpaka anastaafu.Naombeni msaada kwenye mchanganuo wa tozo ya 6% na 10% iliyokua inatozwa na bodi ya mikopo ambayo Mheshimiwa rais alizisamehe siku ya may mosi. Nataka kujua utofaut wake upoje na zilkua zinatozwaje?
Yeah, kulingana na kiasi ulichobaki nacho.!Kwahiyo
Kila mwaka deni lilikua linaongezeka?
Sina hakika Kama kutakuwa na badiliko lolote katika hiliNinachokijua ni kwamba 10% ni pale ambapo ulikuwa unachelewa kutoa taarifa ya kuanza kukatwa mkopo,mfano sheria ya bord inasema ukipata kazi unatakiwa ukae miaka 2 ndoo uanze kukatwa na wakati mwingne hiyo sheria walikuwa hawaifuati,ukimaliza chuo na ukapata kazi haraka sana wanaanza kukata .Sasa Sasa kulingana na hiyo sheria ya miaka miwili ikipita haijarishi una kazi au hauna kazi wanaanza kuongeza asilimia 10% kwenye mkopo wako kila mwaka unaochelewa kulipa na ndoo maana mnufaika alikuwa anaweza kulipa mkopo mpaka anastaafu.
Kuhusu kuongezeka kwa thamani ya pesa yao 6% nayo ni kila mwaka make wanadai pesa yao inaongezeka thamani ,fedha waliyokupa 2010 mpaka unamaliza kuilipa 2025 itakuwa ishaongezeka thamani lwahiyo nani alipie?, Kwahiyo mama yetu ameyaona haya na akaamua kuondoa.Na inaanza mwezi wa saba kwahiyo usipoona mabadiliko ni kwenda kwenye ofisi zao na kupigiana maisabu ili upate mkopo wako halisi na makato unayostahuli kulipa kwa kila mwez.
Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Kwa kuwa zimeshafutwa basi.., tugange yajayo..!!Naombeni msaada kwenye mchanganuo wa tozo ya 6% na 10% iliyokua inatozwa na bodi ya mikopo ambayo Mheshimiwa rais alizisamehe siku ya may mosi. Nataka kujua utofaut wake upoje na zilkua zinatozwaje?
Asante mama Samia mitano tenaSina hakika Kama kutakuwa na badiliko lolote katika hili
6% iliyoitwa kihuni retention fee ya mwaka wa kwanza wa marejesho na 10% ya ucheleweshaji waliviingiza kihuni kwenye deni la mwanzo
Hata hivyo kila mwaka hii 6% ilikuwa inakuwa calculated na kuwekwa kwenye mfumo "uliojificha" wa loan board mnufaika hakuwa na uwezo wa kuona kinachoongezeka kila mwaka
Mnufaika aliendelea kukatwa deni la Mwanzo (yaani mkopo halisi + 6% retention fee ya mwaka alioanza marejesho + 10% ya penalty Kama alichelewa kuanza) bila kujua kuwa ana deni lingine linaloongezeka kila mwaka bila kujua
Kwa hiyo possibility kubwa ya kilichofanyika na Waziri ni kuondoa hii 6% ya ongezeko la kila mwaka lakini waliyoongeza mwaka wa kwanza hawataiondoa
Pia hii penalty ya 10% nadhani wataondolewa ambao hawajaanza makato
Kwanini nasema hivi?
Hii retention fee ya 6% ya ongezeko la kila mwaka ilianza kupigiwa kelele pale lilipojulikana rasmi baada ya baadhi ya wadau kumaliza deni halisi la kwenye salary slip (lililoingizwa na hazina la mkopo halisi + retention ya mwaka wa kwanza+ penalty)
Wanafaika mara baada ya saraly slip kusoma NIL kwenye loan board waliitwa na maafisa utumishi kupewa nakala ya deni jipya!
Walipolalamika walielekezwa wapeleke malalamiko loan board na huko wakajibiwa kuwa kulikuwa na ongezeko la 6% kwa kila mwaka na hili ongezeko lilikuwa haliwekwi kwenye mfumo wa hazina, lilibaki loan board.
Hivyo ulikuwa ukimaliza tu, wanakuprintia deni jipya na hilo deni linakuwa na ongezeko la asilimia sita kila mwaka. Hiki ndo kinaenda kuondolewa
Huu ndio ulikuwa wizi wa wazi. Ule mkopo hadi unachukua na kuanza kulipa ni mkataba. Bodi ya Mikopo wanapokuwa wanapeleka Deni la kulipwa kwa mwajiri inamaana wamekiri kuwa hilo ndio deni halisi la mdaiwa kama wafanyavyo watu wa benki. Sasa inakuwa ajabu mtu umekatwa deni lote la 10M kwa mfano halafu baada ya miaka kadhaa ya mateso ukimaliza unamshukuru Mungu angalau upate unafuu, ati wanaibuka na deni lingine ambalo walikaa nalo wao tu peke yao uanze kulipa. Tena unaweza kuwa umenaliza kulipa deni halisi hata miaka 5, wao wanaliongeza wanavyotaka ili uje ulilipe nyingi baadae. Kwa kweli tumeonewa sana. Jawa jamaa wanapaswa wachunguzwe vzr, huenda kuna magumashi walikuwa wanatufanyia. Hakunaga utaratibu wa kuficha deni nje ya lile mlilokubaliaba na kumfikishia mwajiri kwa ajili ya makato.Sina hakika Kama kutakuwa na badiliko lolote katika hili
6% iliyoitwa kihuni retention fee ya mwaka wa kwanza wa marejesho na 10% ya ucheleweshaji waliviingiza kihuni kwenye deni la mwanzo
Hata hivyo kila mwaka hii 6% ilikuwa inakuwa calculated na kuwekwa kwenye mfumo "uliojificha" wa loan board mnufaika hakuwa na uwezo wa kuona kinachoongezeka kila mwaka
Mnufaika aliendelea kukatwa deni la Mwanzo (yaani mkopo halisi + 6% retention fee ya mwaka alioanza marejesho + 10% ya penalty Kama alichelewa kuanza) bila kujua kuwa ana deni lingine linaloongezeka kila mwaka bila kujua
Kwa hiyo possibility kubwa ya kilichofanyika na Waziri ni kuondoa hii 6% ya ongezeko la kila mwaka lakini waliyoongeza mwaka wa kwanza hawataiondoa
Pia hii penalty ya 10% nadhani wataondolewa ambao hawajaanza makato
Kwanini nasema hivi?
Hii retention fee ya 6% ya ongezeko la kila mwaka ilianza kupigiwa kelele pale lilipojulikana rasmi baada ya baadhi ya wadau kumaliza deni halisi la kwenye salary slip (lililoingizwa na hazina la mkopo halisi + retention ya mwaka wa kwanza+ penalty)
Wanafaika mara baada ya saraly slip kusoma NIL kwenye loan board waliitwa na maafisa utumishi kupewa nakala ya deni jipya!
Walipolalamika walielekezwa wapeleke malalamiko loan board na huko wakajibiwa kuwa kulikuwa na ongezeko la 6% kwa kila mwaka na hili ongezeko lilikuwa haliwekwi kwenye mfumo wa hazina, lilibaki loan board.
Hivyo ulikuwa ukimaliza tu, wanakuprintia deni jipya na hilo deni linakuwa na ongezeko la asilimia sita kila mwaka. Hiki ndo kinaenda kuondolewa
Aisee inaumiza sana jamani!Huu ndio ulikuwa wizi wa wazi. Ule mkopo hadi unachukua na kuanza kulipa ni mkataba. Bodi ya Mikopo wanapokuwa wanapeleka Deni la kulipwa kwa mwajiri inamaana wamekiri kuwa hilo ndio deni halisi la mdaiwa kama wafanyavyo watu wa benki. Sasa inakuwa ajabu mtu umekatwa deni lote la 10M kwa mfano halafu baada ya miaka kadhaa ya mateso ukimaliza unamshukuru Mungu angalau upate unafuu, ati wanaibuka na deni lingine ambalo walikaa nalo wao tu peke yao uanze kulipa. Tena unaweza kuwa umenaliza kulipa deni halisi hata miaka 5, wao wanaliongeza wanavyotaka ili uje ulilipe nyingi baadae. Kwa kweli tumeonewa sana. Jawa jamaa wanapaswa wachunguzwe vzr, huenda kuna magumashi walikuwa wanatufanyia. Hakunaga utaratibu wa kuficha deni nje ya lile mlilokubaliaba na kumfikishia mwajiri kwa ajili ya makato.