Nauliza kwa wanaofahamu: Je inawezekana Juice dispenser ya mitungi mitatu kuendeshwa kwa solar?

zeuman

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2023
Posts
265
Reaction score
501
Wakuu habari za kazi. Nina juice dispenser ya mitungi mitatu, lakini ilitengenezwa maalumu kwa kutumia umeme. Nataka kwenda kuitumia mahali ambapo hakuna umeme, ndipo nikawa najiuliza je inawezekana nikanunua mfumo wa solar na ikawezekana kuiendesha hiyo juice dispenser?
Specification zake ni: Rated input 500W, Voltage 220V-240V.

Je kama inawezekana, ninunue panel ya ukubwa gani na betri ya ukubwa gani na inverter ya ukubwa gani? Naomba sana mwenye ushauri wa kitaalam katika hilo.
 
Mh? Mkuu! Tembelea wauzaji wa mifumo ya umeme wa solar! Hata hivyo umeme wa solar ni "direct current, dc"; na umeme wa TANESCO ni "alternating current, ac". Basi, utahitaji "inverter", kama hicho kifaa chako akina option ya dc
 
Asante! Bali ningependa kama kuna ambaye atanipa maelekezo ya uhakika ili kwanza nijue kama inawezekana kisha itanifaa ipi halafu nafunga safari kwenda kunua kitu ambacho tayari nina maelekezo yake ya uhakika. Hii ni hatua ya mwanzo, mwisho wa siku nitafunga safari kwenda kununua.
 
Piga picha mahali penye maandishi ya aina ya umeme na mahali unapoingizia umeme wa hicho chombo chako utuwekee hapa itakuwa vizuri kukushauri
 
Specification zake zilizoandikwa pale ndo nimezinukuu hapa:
Voltage AC 220-240V
Rate 500W.
 
Mkuu,
Kwanza kabisa hapo utahitajika kuwa na Kifaa kiitwacho Inverter ambayo iwe na uwezo wa zaidi ya hizo 500W, na mara nyingi zipo zenye 750W. Hapo utahitajika kupata solar panel kubwa pamoja na battery zenye storage kubwa ya chaji, ili angalau kuweza kuihudumia hiyo 500W dispenser kwa masaa machache.
Kama kuna uwezekano ni bora utafute chanzo cha kupata umeme wa AC (Alternating Current) moja kwa moja ,kuliko huu wa DC (Direct Current). Umeme wa solar huwa na ufanisi zaidi ukiutumia hivyo hivyo kwenye DC bila kuufanyia conversion. Aidha ni vema mtumiaji wa Sola kutafuta vifaa vinavyotumia umeme wa DC.
 
For optimum design one should provide working hours per day.

Unlike TANESCO, Solar energy is finite. Working hours per day helps avoid under/over engineering.
 
Back
Top Bottom