Nauliza kwanini hatuna safari za meli Mtwara to Dar

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Je, ni wafanyabishara wa mabus wanahujumu? Mbona nchi zilizoendelea huko tunaona usafiri aina zote unaendelea meli, treni na mabus yanapiga kazi vilevile.

Kwanini huku miradi hii inasua sua Kwa mfano mafuriko yaliyoharibu barabara ya Kilwa Lindi huko kupelekea watu kuzunguka njia ya Songea pale kama meli ingekuwepo watu wangeenda Dar Kwa njia ya bahari.

Kwanini meli zinabakia kwenye maziwa tu.
 
Wakati Wa Hayati Mkapa Ilikuwepo Meli Inaitwa Santorino Inatoka Dar Es Salaam ~Mtwara Via Lindi Sijui Kulitokea Nini Ikaondoka
Dar ~ Bagamoyo Jiwe Alinunua Kifuko Kizee Kikawa Siku Nzima Kinahaha Baharini
Akakipeleka Jeshini
 
 
TACOSHILI...Tanzania Coastal Shipping Line ni shirika la meli lililokuwa na jukumu la kutoa huduma ya usafiri majini kwenye mwambao wote wa bahari. Ili kufika Mtwara enzi zile za Muasisi ililazimu kuabiri meli za shirika tajwa lakini baadaye hata meli za Zanzibar zilifanya safari za Mtwara.
Mkanganyiko wa ubinafsishaji ndio uliokuja kuua mashirika na makampuni ya umma hadi sasa ambapo uwekezaji mkubwa kama huo hufanywa na wątu binafsi lakini kwa baraka za chama cha zamani.
 
Mbona Dar kwenda Zanzibar zipo safari nadhani hakuna mwamko wa kusafiri kwa meli
 
Hivi,kwa wastani kutoka Dar kwenda Mtwara kwa meli,safari hiyo huchukua muda gani kufika?
 
Zaidi ya masaa 14..kwa zile meli zilizotajwa hapo juu zilikuwa zinatoka Mtwara saa 10 jioni zinafika Dar saa tano asubuhi siku inayofuata.
Halafu kulikuwa na uhuni wakiona vyakula ndani ya meli havijanunuliwa na abiria wataichelewesha hiyo meli ili kuwatia njaa.
Kwa wakati huo kwa vile barabara haikuwa na uhakika ambapo ungeweza kutumia siku tatu hadi wiki moja(wakati wa masika) meli ilionekana nafuu,kwa sasa labda zije meli za mwendo kasi ambazo zitaenda chini ya masaa 6 kwani mabasi yanatumia masaa 8 hadi Mtwara.
Hivi,kwa wastani kutoka Dar kwenda Mtwara kwa meli,safari hiyo huchukua muda gani kufika?
 
Wewe unaweza kusafiri masaa 14 Dar-Lindi/Mtwara? Meli zimekufa natural death baada ya barabara kuwa nzuri. Meli zilikuwepo unasafiri usiku kucha nani ataweza sasa hivi? Labda zije meli za starehe una safiri kwa starehe sio safari zetu za kupambana kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…