Nauliza, na nyie huwa mnaangalia Bunge huko kwenu?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Ningependa kufahamu kama huu ni ugonjwa wa TZ tu au labda pia huko Kenya upo kwamba watu hawana kingine cha kufanya isipokuwa kufwatilia Bunge?

I mean, hapa Bongo nchi nzima husimama kipindi Bunge likianza, najua ni kwa sababu Watanzania wengi hawana hobby ndo maana huishi kwa matukio, vipi na Kenya ni hivyo hivyo au watu wana maisha yao nje ya Bunge?
 
Kenya kuna BungeTv na SenateTv ila wakenya huwa wanafatilia yaliyojiri bungeni, jioni baada ya kazi, wakati wanatizama habari. Au mara moja moja wakati kuna miswada ambayo inaleta utata.
 
KBC huwa inaleta live procedings za bunge hivyo kuna watu huwa wanatazama...mimi huwa natazama mara moja moja mfano rais akiwa anahutibia wabunge bungeni...kisha sioni makosa watanzania wanapo fatilia bunge...nadhani hio ni haki yao na ni jambo la busara pia...kujihusisha na mambo yanayojiri serikalini ni jambo nzuri tu...pengine uniambie hutaki kujua wabunge wanatumia hela zako kivipi..miswada mengine yanayopitishwa bungeni yanaweza kuku impact kwa njia moja au jingine hivyo watz waendelee kutazama tu...
 
Sasa hapa unaingilia uhuru wa Watanzania wenzako, maana waangalie wasiangalie haikuhusu wewe binafsi maana una kwako na majukumu ya kwako. Kwani taarifa za bunge zinapeperushwa kusudi zitazamwe na mbuzi/kondoo au watu.
Wakenya huwa tunachakarika kikazi, lakini kunao hufuatilia haya mambo na siwezi kuwabeza au kuwasimanga maana wanajielewa na wana sababu na haki zao na ni uhuru wao kutazama yanayojiri ndani ya nchi yao.

Cha msingi kila mmoja wetu anayo majukumu ya kwake ya kuwapelea familia yake mkate wa kila siku.
 
Hapa Kenya watu wengi hufwatilia kukiwa na mjadala moto moto, siku zingine za kawaida watu huangalia tu channel zingine.
 
mtoa uzi she look a stupid cunt#

Duh! Hamna haja ya kumtukana matusi mazito, hivi JF mbona watu wengi mnashindwa na uzalendo au uvumilivu, kila mtu analogin kutoa maoni yake, kama ukiona maoni ya mtu fulani yana ukakasi, au yupo chini ya level yako unamtia kwenye block list, kuanzia hapo hutaona anachoandika, kunao kadhaa nimewatia kwenye ignore list maana wapo humu kutusi tu, unakuta mtu hajadili hoja, anajibu kila hoja yako kwa matusi.
Unamtia kwenye block kuanzia hapo hata atusi vipi, inakua kama mbwa anayebweka bila meno, maana sioni chochote anachoandika, mfumo wa JF una whitewash kila comment yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…