Pole sana kwa hiyo changamoto.
Ushauri wangu: usibadili jina kwa sababu tu baba yako hakutambui kama mwanaye.
Baba yako anaweza akawa hakutambui, lakini ndugu zake wanaweza wakawa wanajua ukweli kuwa wewe ni mtoto wa "baba yako"
Hata kama baba yako hakutambui kama mwanawe, ndugu zako hawataacha kukutambua kisa tu baba yako kakukataa
Isitoshe, kama yeye amekataa kukutambua, wewe amua kumtambua hata kama hamuwasiliani. Iwe mnawasliliana au hamuwasiliani, bado ataendelea kubaki baba yako. Hata ukibadili jina, bado utaendelea kubaki mwanaye wa damu ikiwa ndiye aliyekuzaa.
Kwa hiyo, usibadili jina kwa sababu hizo. Labda kama kuna sababu zinginezo.