Naulizia biashara ya Tractor

Prince Funny

Member
Joined
Feb 14, 2015
Posts
7
Reaction score
0
Naulizia mwenye kuifahamu vizuri Biashara ya kukodisha Tractor kwa kulimia, wakulima anieleweshe taratibu zake. Nataka kufanya Biashara hii, Ni mikoa gani inalipa sana?
 
Kwa hiyo umejiandaa kufanya biashara ambayo hujafanya utafiti hata kidogo?
 
Naulizia mwenye kuifahamu vizuri Biashara ya kukodisha Tractor kwa kulimia, wakulima anieleweshe taratibu zake. Nataka kufanya Biashara hii, Ni mikoa gani inalipa sana?

Naifanya hiyo biashara ni nzuriasana ila inataka uwepo mwenyewe au umpate mtu muaminifu zaidi ya Malaika ila ni biashara nzuri na pia Inategemea aina ya tractor.sijajua tractor yako ni aina gani maana unaweza kununua tractor ukawapa watu lawama watakao isimamia nijibu hapo halafu nifunguke zaidi ni aina gani ya tractor na unampa mtu asimamie au wewe
 

Nategemea kununua Massey 440 . ninaconection UK. Hivyo naiagiza tokea huko na ninataka kuifanya mwenyewe
 
Nategemea kununua Massey 440 . ninaconection UK. Hivyo naiagiza tokea huko na ninataka kuifanya mwenyewe

Ni biashara nzuri sana ila huyo unayemuagiza angeweza kupata Model ya 165, 175, 185, 255, 260, 290, hizi nimezitumia ni nzuri na spare nafuu sana na zinahimili shida.msimu unaanza mwezi wa 9 unaanzia mahenge morogoro kule kuna mbuga zinaanza kulimwa wkt hakuna mvua utalima hadi mwezi wa 12.pale unaipakiza ktk Fuso unaenda Kiteto kiteto unalima kuanzia mwezi wa 12 hadi wa 3.sasa msimu wa kiteto unapokalibia kwisha unasogea Handeni Tanga pale inatembea yenyewe Tanga unalima mweziwa 3 hadi wa 44.msimu ukiisha unaitafutia trailer na mashine ya kupukuchua mahindi kwa hiyo mkulima utampukuchulia atakulipa utambebea atakulipa pia ni biashara nzuri sana mimi nimenyanyukia huko na bado naifanya inalipa ila uwe mwenyewe. Km una swali uliza mkuu ntakupa mpaka kiasi heka inatakiwa ulime kwa udongo wa mahenge kiteto na Tanga
 
Thanks for info kiogwe. Ila ninaswali jingine je hizi model ulizotaja zinatumiaje mafuta kwa heka? Na kwasiku zinaweza kulima heka ngapi? Na je service zake baada ya masaa mangapi na kiasi gani?
 
Thanks for info kiogwe. Ila ninaswali jingine je hizi model ulizotaja zinatumiaje mafuta kwa heka? Na kwasiku zinaweza kulima heka ngapi? Na je service zake baada ya masaa mangapi na kiasi gani?

Ili tractor ikulipe vizuri inatakiwa isizidi lita 4 kwa hekari moja na kwa hekari inategemea na udongo mfano kwa Ifakara na Mahenge inatakiwa upate heka zisizopungua 20 kwa siku na jitahidi hata wafanye kwa masaa 16 kwa siku na kwa tractor used inaweza bila shida ila kwa hizi za jeshi za kilimo kwanza nazani haziwezi sina uhakika sana.servise inategemea na aina gani ya oil unatumia km unatumia oil mbovu masaa ya servise yatapungua mimi natumia total oil kwa udongo mzito nabadili oil kwa heka mia na hamsini kwa udongo mwepesi nabadili kwa heka mia 2
 
Ila kwa swala la oil bado sijampata mtaalamu anisaidie vizuri nibadili vipi km kuna mtaalamu humu anisaidie kunielimisha nibadili muda gani kitaalamu na oil gani nzuri kwa chombo maana nina safari ya Mtwara msimu ujao siendi kulimia watu naanza na mashamba yangu na pia km kuna watu wa bank watupe mawazo nahitaji kulima ekari mia 4 ya ufuta nina tractor ntapataje mkopo wa pembejeo mbegu na madawa
 

Akhsante tena kwa muongozo mzuri. Nami ngoja nisuborie mtaalam wa mitambo watuambie aina ya oil ya kutumia na kwa heka ngapi au masaa mangapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…