Habari za hapa Jamvini wakuu.
Natumai mu-wazima kabisa na bila ya kupoteza muda ningependa kueleza shida niliyo nayo ni kama MADA inavyosema kuwa nahitaji kampuni itayoweza kusafirisha mizigo kwenda Congo.
Ningependa kujua taratibu za usafirishaji pamoja na charges zake pia zikoje,mzigo unaosafirishwa ni maziwa ya unga mfano wa COWBELL bag ya 25kg kwa bags 200.
Yeyote mwenye kufaham au mwenye kampuni ya kusafirisha ningependa kufaham yaliyoainishwa hapo juu tafadhali,KARIBUNI.
huo mzigo mdogo,kupata transporter wa magari makubwa kama semi ni ishu,kwani mengi yanatoka bandarini na mzigo full,hawawezi ongeza mwingine juu kwa kuhofia mzani.
labda utafute fuso
Kuna hawa mabwana, ni wasafirishaji wasiliana nao,ila sijajua uko mkoa gani
Shukran kiongozi mi niko Dar na mzigo unatokea Dar pia nimeona hiyo attachment hapo kiongozi naona kuna phone number na P.o.box na jina la Kampuni tu hakuna details zozote zinazoihusu kampuni husika.....................mi niko Dar kiongozi labda sjui pengine unawafaham hao jamaa au umewakuta tu mtandaoni kiongozi ?,SHUKRAN.
Mimi ni Architect, nilipata kuwachorea moja ya yard zao za kupaki Horses(vichwa vya truck) na kusimamia ujenzi wake...kwa hiyo ni watu naowafahamu! Yaate ni kifupisho cha Yasin Abdul Tengegu ambaye ni director! Kuweka namba za simu maanayake upige ditails nyingine watakupa maana kampuni mbali na transportation wanajihusisha na kazi nyingine! Wapo Sinza - Sekilango RD ukitokea sheli ya Puma(zamani BP) Kabla hujafika Mugabe kuna Jengo la ghorofa upande wa kushoto lenye vioo upande wa mbele! Wako floor ya nne/tano kama kumbu kumbu hazijaniendea kushoto

Mkuu hao Yaate sio msaada kwake.Yaate anasafirisha mizigo iliyo ktk ma container zaidi zaidi akienda hapo watamfanyia udalari watamtafutia fuso.kuna mdau kasema atafute Fuso ni kweli hebu nenda pale kurasini shimo la udongo uliza yard ya malawi cargo huwa kuna wafanyabiashara wa nchi mbalimbali wanaponunua mzigo huwa wanachanga na kusafirishwa na gari 1 ni madalari flani lakini ndio msaada wako upo hapo.hata kama si hapo utaelekezwa uende wapi
Habari za hapa Jamvini wakuu.
Natumai mu-wazima kabisa na bila ya kupoteza muda ningependa kueleza shida niliyo nayo ni kama MADA inavyosema kuwa nahitaji kampuni itayoweza kusafirisha mizigo kwenda Congo.
Ningependa kujua taratibu za usafirishaji pamoja na charges zake pia zikoje,mzigo unaosafirishwa ni maziwa ya unga mfano wa COWBELL bag ya 25kg kwa bags 200.
Yeyote mwenye kufaham au mwenye kampuni ya kusafirisha ningependa kufaham yaliyoainishwa hapo juu tafadhali,KARIBUNI.
Asante mkuu kwa ushirikiano wako kiongozi na je ukiacha haya yanayotoka bandarini full,nadhani pia kuna kampuni tofauti tofauti huwa zinasafirisha mizigo ya mtu zaidi ya mmoja kwa pamoja hata hizo zinatosha si lazma nikodi gari zima ili nijue wata-charge kiasi gani.
Na kama ulivyosema nichukue fuso nafkiri wengi wao huwa wanasafirisha ndani ya nchi let say Kigoma na mikoa tofauti nafkiri zipo ambazo zina vibali maaalum kwenda nchi jirani na sidhani kama inawezekana tu kuchukua fuso lolote na kusafirisha mzigo hata kama kibali chake hakimruhusu kusafirisha nchi jirani, HIYO IKO VIPI WAKUU ?.
Kama ni bags 200,unaweza kuchukua hata Fuso ambayo ni Transit,na kama ni macontainer nitwangie 0687089078
Fuso za kwenda Transit zipo
Nashkuru kiongozi i hope utakuwa kwenye hiyo sekta mkuu huwezi kosa connection ya mtu wa trip kama hizo kiongozi una namba ya mtu mwenye hizo gari ambazo ni transit unisaidie mkuu ?.