Naumia, nami ni binadamu

Naumia, nami ni binadamu

Nimekuelewa
Pole sana mkuu.
Kwanza ingekuwa mimi ndio wewe nisinge funguwa uzi wa sonona, na zaidi ningewakaushia kana kwamba siwajui, nakwa roho mbaya nisinge badili hata ID, na pesa zao nisinge warudishia.
Pole kwa changamoto unazo pitia, nakukumbusha tu kwamba hii ndio Jf.
 
Hata ukikaa kimya na kunyamaza bado watasema tu.
Sikushauri kurudisha pesa kwa waliokusaidia vinginevyo endapo mtu aseme ndio anachokihitaji kurudishiwa pesa zake.

Hata baada ya kuandika huu uzi wataendelea kusema tu. Hautawazuia na hilo lipo nje ya uwezo wako.

Ukiweza, watendee wema wenye uhitaji.
 
Ni Mungu pekee awezae kuubadili moyo wako na kuufanya kuwa mgumu,
Kwani akikaa ndani yako na utaenenda kwa jinsi ya kiroho.
Wanadamu hawata kutenda kitu.

Lakini ukitegemea uwezo wako mwenyewe, wanadamu lazima wakuvyoge vyoge na kukuumiza.
 
Masikini pole sana mama, ndio walimwengu tulivyo. Usiwe ma moyo mwepesi wa kubeba mambo kiasi hicho dear. Hii dunia ina mengi na hayo ndio kwanzaaa kumekucha. I feel yo pain na nafikiri niliona hivyo vijembe kutoka kwa wawili wa waliokusaidia ila usipate taabu maana nafikiri tayari unawafahamu ni watu wa aina gani. Haupaswi kuwapa nafasi kabisa ya kuizuia furaha yako.

Hauna haja ya kurudisha hizo pesa, ichukulie tu kama funzo kwako na endelea na maisha yako. Mshukuru Mungu uko na afya njema sasa, muombe azidi kukupa afya ili upambane ufikie malengo yako.
 
Unaumia sababu unawapa attention...! Tenda wema uende zako sasa wao wametenda na hawakuondoka walibaki hapo na wewe ukaona ubaki pale badala ya kuondoka zako uwaache pale. Pole aggyjay kwa masaibu.
Kwa marafiki na jamaa wa jf.
Mwaka 2018 nilipata tatizo la ghafla na kuugua,na pia sikua na uwezo ama kujiaandaa kukabiliana na hill tatizo.kwani nlitoka kwenye kipindi kigumu cha kumuuguza ndugu yangu na sikua na kipato,hali ilivozidi kuwa mbaya ikanilazimu kuomba msaada kwa baadhi ya marafiki wa jf,kuna watu walijitokeza na kunisaidia kupata 300K ya bima ya Afya nkaleta na mrejesho
Lakini tatizo liko hapa;
Kuna baadhi ya member mnaniweka kwenye masikitko na huzuni,its like Mimi ndo wa kwanza kupata matatizo na kuomba msaada jf?
Imekua too much kwa sasa,lisitokee jambo mtu kaibuka na kuongeea msaada nliopata,kuna wengine mnafikia hata ya kunidhalilisha kwa makosa yasiyojulikana,makosa ambayo siyajui na hapana ukweli kabisa.

Kuna mda mwingine nakubali nakosea,nakubali na naomba mkumbuke Mimi ni binadamu kama wengine sio malaika.
Lakini kinachoshangaza na kuumiza mtu anakuja na kuingiza habari za msaada kwenye hayo masuala..its inhumane.
I appreciate what you did to me,ni kitu kikubwa ambacho kilinisaidia mno,lakini the way mnavolikuza na kuliongelea ni kama nlipewa mkopo na si msaada wa kibinadamu..
Whenever you get a chance u use it to insult me..why!
Mimi ndo wa kwanza kuomba msaada humu jf?kama kwenye matatizo wore wangetreatiwa hivi ni yupi angekua na amani mbele za watu?
guys,nlipoteza wazazi wore wawili nkiwa mdogo sana.nkachukuliwa na familia ya mtu,nkakua kwao,lakini kila nikikosewa au kufanyiwa ubaya kama binadamu nkiongea kuonyesha nlivokereka maneno ntayorudishiwa ni "huna baba wala mama,tumekulea hadi umekua nk.!
Nnapopokea kauli kama hizi natamani nifanye malipo,angalau kupunguza maneno,,lakini malipo ya wema na utu ntayalipaje,kama ni chakula ntawalisha nkifanikiwa.
Na kwenu pia,nashukuru sana kwa mda wenu,kujitoa kwenu na upendo wenu mlioonyesha.wenyezi Mungu Atawalupa kwa hili.
Lakini kwa upande wa pesa angalau ntawalipa.nko imara kwa sasa hapo sio kikamilifu lakini nna nguvu ya kufanya mengi ukilinganisha na mda uliopita.
Ntajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu nirudishe kidogo kidogo angalau maneno yapungue.maana najiona nna deni kwa jinsi hali ilivo.

Watu walionifanikisha msaada wapo 13.kipindi napokea msaada niliwanote kwenye diary, na wote nawajua I'd zao na amount ya kila mmoja.ntajitahidi taratibu kurudisha angalau nipate nafuu.
Nawapemda wote!
Aggy!
 
Ushauri wangu usirudishe ulichosaidiwa kama waliokusaidia hawajadai utakuwa unakosea. Hao wanaokudhihaki kwa shida ulizopitia kipindi cha nyuma iko siku yao. Hakuna anayependa kusaidiwa ila inafika mahali akili inagota kabisa unashindwa ufanye nini kutatua shida yako. Ipo siku yao ni heri wakaomba msamaha saa hii kuliko watacholipwa na Mungu wanaemuamini. Nimeandika haya kwa uchungu sababu nimewahi kupitia changamoto kama zako nimesaidiwa sana hata sasa bado nasaidiwa napokwama.
 
Write your reply... Ama hakika, umenisikitisha sana, au kuna baadhi yao walikusaidia wakijua watapata kitu kutoka kwako lakini ukawabania?

sikiaaaa sasa! hamna kurudisha hata mia hapo hao wanafik tu, kama vp change na username yako wasikuzoee tena_ na usiwe na mawasiliano nao hao ni wahuni sista.

nimetamani sana kujua mengi kuhusu wewe, ama hakika historia yako imenigusa sana.

KING OF THE JUNGLE!
jtj
 
Hata ukikaa kimya na kunyamaza bado watasema tu.
Sikushauri kurudisha pesa kwa waliokusaidia vinginevyo endapo mtu aseme ndio anachokihitaji kurudishiwa pesa zake.

Hata baada ya kuandika huu uzi wataendelea kusema tu. Hautawazuia na hilo lipo nje ya uwezo wako.

Ukiweza, watendee wema wenye uhitaji.
Sawa mkuu
 
Write your reply... Ama hakika, umenisikitisha sana, au kuna baadhi yao walikusaidia wakijua watapata kitu kutoka kwako lakini ukawabania?

sikiaaaa sasa! hamna kurudisha hata mia hapo hao wanafik tu, kama vp change na username yako wasikuzoee tena_ na usiwe na mawasiliano nao hao ni wahuni sista.

nimetamani sana kujua mengi kuhusu wewe, ama hakika historia yako imenigusa sana.

KING OF THE JUNGLE!
jtj
Asante mkuu,hasa ukiangalia wengine wanashusha shutuma,halafu si za kweli kabisa.its embarrassing.
Kuna watu wana dharau.
 
Back
Top Bottom