Naumizwa sana na namna ambavyo TISS inakuwa ni ya siri kweli kweli, vijana ambao tuna project zetu sometimes tunahitaji sana support yenu

Natamani tuwe kama wachina, Russia au Iran. Katika vitu nyeti kunakuwa na mifumo yetu sio mifumo ya nje.
We jamaa unanichekesha ushapona kitu gani nyeti????

Ushapona tulitumia mifumo ya wazungu kwenye kitugani nyeti?
 
TISS hawawezi kukusaidia chochote.

Wenye uwezo wa kukusaidia chochote ni Wanasiasa wenye madaraka tu.
 
Natamani tusitumie mifumo ya kizungu. Ma develooer wa kibongo sijui wanafanya nn sio wabunifu. Kama fb, twitter tunatakiwa na sisi tutumie za kwetu ili kulinda data zetu
Jamii forum
 
Hahah, hao watu kama uliyemtaja, ni janjajanja ya kujua kuongelea products za wazungu tu na kuwatafutia masoko, hakuna talent yoyote hapo sanasana wana exposure tu.

Yes wazungu wanawatumia ndio lakini si kuwatengenezea mifumo, la hasha, bali wanawatumia kuwatangazia bishara zao. Ikiwa hichi ndio unacholilia hapa, basi bado hujaelewa jinsi teknolojia inavyokimbizwa pamoja na fitna zake.

Niliwahi hudhuria semina moja iliandaliwa na hao/huyo uliyemtaja, semina ya siku 5 zote ni makampuni ya kizungu tu yalitangaza bidhaa zao kwa ajili ya Cyber Security, vitu kama Firewalls, Routers, Forensics tools nakadhalika, wadau ni makampuni ya IT na taasisi za serikali, hao watanzania wanachokijua ni concepts na kushawishi makampuni na taasisi kununia hizo bidhaa, in other words ni agents wa wazungu.

Unachokizungumzia wewe kwenye mada yako (Nzuri) ni Tanzania kama nchi ikae chonjo kwa kuandaa mifumo itakayotumiwa kama mbadala wa mifumo ya wazungu, well, naamini serikali inajua, sana tu, lakini hebu tuliangalia hili jambo kiuhalisia, unadhani ni rahisi?

Je wewe huo mfumo ulionao au ulioutengeneza hautumii frameworks/platforms/libraries za wazungu? Unajua hizo codes zinafanya nini in and out? Hardware utakazotumia ku deploy huo mfumo wako sio za wazungu? Unafahamu in details how they work when communicating? Unafahamu politics zilizopo kwenye biashara za kiteknolojia? Hivi Tanzania tuna huo uwezo?

Mi nadhani tunahitaji kua na sera pamoja na miongozo mizuri ya kudhibiti matumizi ya hii mitandao na tuwe wazalendo kufuata miongozo hiyo, ila kuwakwepa moja kwa moja wazungu kwenye mifumo yao bado tuna safari ndefu sana, na tunahitaji uwekezaji mkubwa mno.
 

Asante kaka nmekuelewa sana. intelinside ndomana wachina wana fight kutengeneza cheap zao. Pamoja na operation system zao. Ila mm nilikuwa namaanisha tuandae mazigira ya vizazi vyetu vijavyo. Mfano tu. Utakuta watu wa serikali wanatumiana private doc ktk whatsapp. Kuvuja zinakuwa rahisi
 
Mkuu Hii nchi ina wenyewe wenyewe ni Fisiemu Fisiemu ndo wanaowapigia panga ndgu zao na jamaa nafasi nzuri kama hizo sasa ww kajamba nan mwenzangu wap na wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…