Naumwa naombeni msaada wa tiba mbadala.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Wakuu habari zenu!
Jamani miye naumwa upande wa kushoto wa moyo; nina maumivu makali. Nimekwenda hospital nyingi sijapata suluhisho; maumivu hutulia kwa muda baada ya tiba na kuanza tena. Nashindwa kuelewa ugonjwa huu jamani wengine wanasema ni Angina, wengine dalili za moyo, wengine Uric acid,, ulcers na majina mengi tu. Nisaidieni mnaojua tiba mbadala wakuu. MziziMkavu na wengine nawakaribisha...!
 
Last edited by a moderator:
Pol e sana kwa kuumwa tunweza kukusaidia kwa tiba mbadala lakini hatujaujuwa ugonjwa tutaweza vipi kukupa dawa? ningelikushauri uende Hospitali ya muhimbili ukapige XRay na pia upime Damu ili wapate kujuwa Ma-Daktari unaumwa ugonjwa gani? Ninakupa huduma ya kwanza (first aid) Kama unayo nyumbani Asali kunywa kijiko 1 asaubuhi kabla ya kula kitu na wakati wa mchna pia kunywa asali na tena na wakati wa usiku kunywa tena Asali huku uende hospitali uje hapa tena utupe majibu ya hospitali wamesema unaumwa kitu gani? uguwa pole Mkuu.@Brightman Jr
 
Pole sana kwa kuumwa. Pia maombi huwa yanasaidia. Fanya sala pia
 
Inawezekana una msongo wa mawazo lkn hujatuambia umepimwa vipimo gani vikaonyesha huna tatizo. Jaribu kufanya vipimo vikubwa hasa waone wataalam wa magonjwa ya moyo . Usisahau kufanya maombi kabla ya kuwaona wataalam Ugua pole mkuu
 
Asanteni kwa ushauri wakuu. Mungu anisaidie nipone maradhi haya!
 
watu wwwa dizaini yako mnaudhi sana, na bado unajiita brightman!

Mkuu ubaya uko wapi kutoa shukrani kwa waliotoa ushauri kwangu? Ndo maana naitwa Brightman, kamwe siwezi kupuuza ushauri wa watu humu jamvini.
 
Pole sana kwa kuumwa. Pia maombi huwa yanasaidia. Fanya sala pia
Ah! We mwache atafute tiba,maombi yanasaidia nini. Kila ugonjwa unadawa yake, hayo maombi nidawa ya ugojwa gani?

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Mkuu ubaya uko wapi kutoa shukrani kwa waliotoa ushauri kwangu? Ndo maana naitwa Brightman, kamwe siwezi kupuuza ushauri wa watu humu jamvini.
watu karibu watatu tumekuuliza daktari ulipoenda alisema unaumwa nini na dawa gani zilikutuliza? maana kuna chanca mbili kubwa angina na ulcers japo panic attack nayo tunaiweka kwa mbali. we badala ya kujibu maswali ya msingi unayapuuza.
 
Mkuu kwa upande wa magonjwa yaliosemwa na madaktari kwa hospitals nilizokwenda nimeyataja pale juu. Kwa upande wa dawa nimetumia nyingi kwa majina si mtaalam;miye nilijua kunywa tu lakini moja sijuwi inaitwa Elgo kit (kulikuwa na aina tatu za dawa hapo). Ndo hivyo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…