Naumwa nisaidieni

Naumwa nisaidieni

Ngala

Senior Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
160
Reaction score
24
Leo asubuhi nilipoamka alfaji kujiandaa kwenda kazini kuzunguzunga kilinishika kama nimeamka na pombe.nikajitahidi nikaondoka kwenda kazini lakini mguu ukawa mzito nauburuza nikiuwekea umakini natembea vizuri nikijisahau tu unaburuzika mbaya zaidi nikiongea utafikiri nimeweka tumbaku mdomoni hata wenzangu kazini walinishangaa wakadhani nimeamka na hangover but wakashangaa hali hiyo ilipoendelea mpaka jioni.wanajf nini tatizo hili na matokeo yake ni nini nanifanyeje. Nisaidieni kabla sijajibinafsisha kitana
 
Pole sna mie sio daktari ila siku iliopita ulikula nn na ulipumzika vya kutosha!! maumivu yakizidi muone Daktari
 
Nadhani umuone daktari mapema iwezekanavyo

Annina
 
Pole sna mie sio daktari ila siku iliopita ulikula nn na ulipumzika vya kutosha!! maumivu yakizidi muone Daktari
Da Mary asante. Nilichelewa kulala na hata jana usiku nimepiga pushup za nguvu na kuruka kichura chura nafuu kwa mbali sana leo asubuhi. Kuhusu daktari nimwone wa maradhi gani
 
Leo umeamka salama? Hiyo kitu inaitwa TIA (transient ischemic attack), ni kwamba sehemu ya ubongo wako ilikosa damu kwa muda. Kwa lugha nyepesi, inawezekana wewe umepata ka stroke kadogo.

Sifahamu una mambo gani katika maisha yako yanayoweza kukuweka hatarini kupata hali kama hiyo lakini ki ujumla "risk factors" zinagawanywa katika zile ambazo zinarekebishika na zile zisizorekebishika.

Zinazorekebishika: Uvutaji sigara, kunywa pombe, viwango vya juu vya lehemu (low density cholesterol) katika damu, ukosefu wa mazoezi (sedentary lifestyle), shinikizo la damu na kisukari

Zisizorekebishika: umri, jinsia (kutegemea na umri)

Ushauri wangu nenda kamuone daktari, hakikisha unaenda kwenye hospitali ambayo una uhakika wa kuonwa walau na Medical Officer na si CO au AMO. Sijui uko katika mkoa/ mji gani.

Kingine unachoweza kufanya sasa hivi kama una Aspirin, meza KIDONGE KIMOJA SASA HIVI. TIA inaweza kujirudia na pia inaweza kutokea stroke kamili hivyo chukua hatua
 
Ngala pole sana, Nenda kacheki damu yako pamoja na presha
 
Injinia ubarikiwe kwa ushauri mzuri
 
na dawa za kiswahili pia kula garlic pills au natural garlic kwa wingi na omega pills ambazo ni mafuta samaki itaisha ila ushauri wa injinia ni real ilishanitokea lakini nadunda
 
Siku chache zilizopita, nilisoma article ihusuyo mambo ya afya na kulikuwa na habari ya dada mmoja kutokewa na hali kama hiyo wakiwa kwenye shughuli ya kifamilia, basi watu wote wakamliwaza na kumpatia maneno ya faraja, kwa kuwa hawakufahamu ni nini kinaendelea basi hat hospitali hawakwenda. Baada ya juma moja yule dada akapata stroke, from which she never had a chance, and the rest is history. Angewahi kwenda hospitali, a life could be saved, so please wahi hospitali na sio kituo cha afya.
 
nawashukuru wanajf kwa maelekezo yenu shukran za ziada kwa injinia mtata.kuhusu nilipo nipo dar na wafanyakazi tunatibiwa hospital ya al ijumaa pale kariakoo.hospital huwaazima madakitari bingwa toka muhimbili sasa sina uhakika kwa tatizo langu kama nitapata daktari bingwa hapo nimepanga kwenda jtatu. ASANTENI SANA
 
Pole sana Mkuu. Inawezekana pia ikawa ni mild stroke lakini kupima damu ni lazima kuhakikisha HB (Haemaglobin) yako okay. Kila la heri. Kwa ushauri tu Mkuu kama unaweza kumuona dr kesho basi itakuwa vizuri sana. J'tatu inaweza ikawa ni mbali sana Mkuu.

http://www.3dchem.com/moremolecules.asp?ID=213&othername=Haemoglobin
 
nawashukuru wanajf kwa maelekezo yenu shukran za ziada kwa injinia mtata.kuhusu nilipo nipo dar na wafanyakazi tunatibiwa hospital ya al ijumaa pale kariakoo.hospital huwaazima madakitari bingwa toka muhimbili sasa sina uhakika kwa tatizo langu kama nitapata daktari bingwa hapo nimepanga kwenda jtatu. ASANTENI SANA

Ngala, please go today. ANYWHERE. Just get your blood pressure checked. And take that Aspirin. It will do you more good than harm (if any). Nakusihi. Jumatatu tusije tukakosa post zako humu
 
Pole sana mkuu jitahidi hiyo jumatatu uende hospital upate ufumbuzi wa tatizo suala la afya ni msingi wa yote.
 
Kwangu hii ni neema kubwa saana kwa mwenzetu kupata ushauri uliomsaidia
 
Back
Top Bottom