Naunga mkono hoja Benchika hafai kufundisha Simba

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Hoja zimeenea leo kuhusu Benchika kutotakiwa, mimi pia naunga mkono kabisa kabisa, Benchika hana uwezo wa kuivusha Simba, Benchika amesababisha mwarabu Al Ahly avunje mwiko kwa mkapa, Benchika amepigwa nje ndani na mwarabu, Benchika amepoteza kombe la CRDB FA cup, Benchika amepigwa zote na Yanga.

Kibaya zaidi, upangaji wake wa kikosi ni hatari sana, yaan anawaweka Sadio, Saido, Ngoma na Babacar, halafu Micquisone akae benchi.

Yaan Micquisone anawekwa benchi bila sababu za msingi lkn akiingia unaona uwezo wake.

Baya zaidi angalien sub za Benchika, unaweza ona Kibu anashambulia wee na amewashika wapinzani lkn Benchika anamtoa.
 
Mwambie Kanjibai weke mzigo asajili wachezaji wa maana level ya akina azizi Ki....Kwa Simba hii hata aje best coach wa dunia kuifundisha mtapigwa nje ndani.
 
Wanayanga hatukubaliani na hoja yenu ya kumng'oa kocha wenu mahili, kocha huyo ametuwezesha Simba na Yanga kufahamiana na kuwa karibu kama wana Dar wa Kariakoo.
 
Kwani huyo Mmakonde akiingiaga sub timu inapata matokeo yapi labda tofauti na anavyoanza Saido?
 
We si ulijitoa kushangilia Simba na kujitoa humu JF kabisa? Kwa wachezaji akina Jobe, hata kocha awe Baba yako hakuna mtakachoambulia. 😀😃😄😁😆
 
Kibu tangia lizi ianze ana goli Moja tu tena kwenye mechi Simba kapigwa 5-1 na kacheza mechi zote za ligi, sasa unataka kocha akomae nae wa Nini sasa, jamaa kajanja sana kakikutana na yanga kanakaza hatari na ndo hapo kawawin makolo
 
HATA UMLETE KOCHA KUTOKA SPAIN KWA WALE WACHEZAJI HUWEZI FIKA POPOTE SIMBA INA KIKOS KIBOVU KUWAHI KUTOKEA
 
Makolo hamjui mnacheza mziki wa YANGA tu miaka yote mitatu. Tulimchana 5 Robatinho,mkamtimua kazi.=(mziki wa YANGA).
2. Mkaenda kumchukua Benchika kisa tu moja kawafunga YANGA 2-1 kwa mkapa. Na kafanikiwa kuchukua kombe kwenye final na YANGA=(mziki wa YANGA).
3. Mkashangilia sana YANGA kupangwa na Memolod mpaka Meck akasema Yes YANGA nae atagongwa 5 na wakubwa wenzie. Na makolo wengi mlijua hivyo. Ajabu mmeshuhudia ball la YANGA likiwapeleka kasi Memolod mpaka kutumia mbinu za kishamba kunyang'anya ubingwa wa YANGA wakimtumia boss wao. Huku makolo mlioshangilia mikishangaa na mpira mwingi wa YANGA,huku nyie miipakatwa IN and OUT =(mziki wa YANGA)
4. Mkachomolewa kwenye CRDB huku mkategemea YANGA nayo inatolewa=(mziki wa YANGA)
5. Mmegongwa 2 jumamosi tayari mmeona Benchika hafai mnataka kumtembeza=(mziki wa YANGA)
6...........
7..........
Mpaka mtakapoacha kucheza mziki wa YANGA. Fuateni yenu
 
Kwa upande wangu Benchika bado ni kocha mzuri na Bora ila Hana wachezaji wenye ubora unaotakiwa wampe muda wamletee wachezaji wazuri watakao ipambania nembo ya Simba hao waliopo Sasa viwango vyao vimeporomoka ghafla hawajitumi.
 
Pale hata aje jose mourinho bado atonekana hafai. Simba hamna wachezaji wenye ubora kwa sasa. Amebaki chama tu labda na che malone ambao nao ubora wao haupnekani kwasababu wamezungukwa na matutusa. Sajilini wachezaji wa maana
 
Naanza kufikiri kuwa huenda CHAMA anakili ya mpira....ukiangalia makocha ambao akipishana nao kimbinu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…