Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Leo nataka nishereheshe moja ya hoja ya Mh. Nape Nnauye Bungeni aliyoitoa tarehe 10 February 2018 ikiungwa mkono na wabunge Mh Msigwa na Mh Zitto Kabwe ya kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa Usalama wa Taifa nchini Tanzania. Nape alitoa hoja hii wiki moja baada ya mimi na yeye kukutana pale Serena Hotel tarehe 5 February 2018 nikampatia kitabu cha Ujasusi na kumuomba akisome, ili alisaidie taifa.
Hoja hii ni muhimu sana sana kuliko inavyofikiriwa, na nihimize wabunge waitilie mkazo bila kuathiriwa na itikadi za kisiasa. Nilisikiliza hata majibu ya Mh Waziri Mkuchika akitetea kwamba TISS haihitaji marekebisho kwakuwa inafanya kazi kwa ufanisi.
Nijaribu kumkumbusha Waziri Mkuchika, mabadiliko ya idara au mashirika ya kiusalama duniani sio jambo geni ama jambo la siri. Tarehe 20 January 1996 Mzee Mkapa alitia saini sheria iliyounda upya chombo hiki cha ujasusi kutoka kuitwa Tawi Maalumu ndani ya Jeshi la Polisi, (SB) na kuzaliwa TISS.
Mzee Mkapa alitumia Bunge hilihili la Jamhuri kufanya mabadiliko haikuwa siri, hakuna mbunge asiyejua kazi na majukumu ya TISS kwakuwa yapo kisheria kwa sheria iliyotungwa na Bunge, Kifungu cha sheria ya Usalama wa Taifa (Duties and Power of TISS) kifungu cha 14-(1),(2),(3) (a) na (b), kinafafanua wazi kazi za MSINGI za TISS. Lakini haiishii hapo tu, kifungu cha 15-(1),(2),(3) (a),(b),(c) na kifungu (4).
Sasa leo Mkuchika akiwapinga wabunge kwa hoja kuwa hawajui kazi za kisheria za TISS inashangaza na huku ndio kuingiza siasa kwenye chombo hiki, kwa Mataifa yaliyoendelea Waziri alitakiwa kutulia na kujibu kwa hoja mujarabu za kimantiki au kupokea hoja za wabunge na kuzipeleka katika vyombo vya michakato kuliko kujibu tu tena kienyeji tu kwa hoja nyeti kama hii.Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi nimeleza kwa kirefu kwanini mabadiliko ya TISS ni muhimu, fuatana nami hapa chini toka kitabuni:
Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 iliyounda upya chombo hiki ina upungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya dunia ya kifikra na kiteknolojia, Sheria hii inaififisha taasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu, sheria inasema, "kazi yake kubwa ni kukusanya na kuchambua taarifa (intelligence gathering and analysis) na kuzipeleka/kushauri wahusika kuchukua hatua."
Kwa maneno hayo, TISS imenyimwa nguvu ya moja kwa moja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu. Mara nyingi utekelezwaji wa aina kama hii ya sheria hufaa kwenye mataifa ya kijamaa na kiimla, lakini kwenye mataifa ya kidemokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi ni hatari sana kuwapo kwa sheria hii. Upitishaji wa sheria hiyo lilikuwa shambulizi moja kubwa dhidi ya mamlaka ya Usalama wa Taifa lililohitimishwa kwa kutekwa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa.
Wanasiasa na mafisadi walifanikiwa, na tangu hapo kuyumba na kudorora kwa taifa kila nyanja ndipo kulipoingia Tanzania. Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi.
Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika kutekeleza wa ushauri wanaopewa na chombo hiki, Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hiyo ili taasisi ya Usalama wa Taifa Tanzania iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe).
Hata hivyo uhuishwaji wa sheria hii ufanywe kwa umakini ili kutofungua mwanya wa idara hii kuwa na nguvu ya kumuondoa kiongozi/rais pia uende sambamba na kuifanya imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii awajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa za vyama.
Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kikanda (regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi. TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni rahisi katika kufanya ubadilishanaji wa taarifa za kijasusi (informations sharing).
wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani, Uingereza, Pakistan, Israel, Afrika Kusini, China, India na Canada.
Ingawa mikakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekuwa ikibadilika kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima ianze na kanda ya Maziwa makuu, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na mpinzani wetu hapa Afrika Mashariki ni Kenya.
Hatujaweza vya kutosha kwenye ujasusi wa kiuchumi (Economic intelligence) kule Kenya ingawa wao wamewekeza hapa kwetu. Leo hii Kenya inasafirisha madini ya TANZANITE, wanasafirisha dhahabu na kadhalika. Uwiano wa kibiashara (Balance of trade) kati ya Tanzania na Kenya ni somo la ujasusi wa kiuchumi kwa nchi ya Tanzania (Economic intelligence).
Tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiintelijensia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie masuala tata yanayoweza kuibuka na mwenendo wa washindani wetu. Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi wa Tanzania hapa Afrika mashariki kupitia Kenya?
Malengo ya TISS kulingana na hali ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri (si utabiri wa majini/tunguri) bali ule wa kisayansi, kupenya, na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu, na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama, kulinda taifa na watu wake, utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye nyanja za kimataifa (jamii nyingine).
Ili kujenga nguvu ya propaganda ya kijasusi, mageuzi muhimu yawe kwenye uhamilishaji wa habari. Lazima ziwepo habari za kijasusi ambazo zitakuwa hadharani, hasa zile ambazo TISS itaamua umma ujue ikilenga kanda ama Afrika zifahamu kwa manufaa ya Tanzania. Ni zile habari tu ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa kufanya kwenye ujasusi wa kiuchumi na upandikizi kiuchumi.
Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi, hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe na Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI). Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio "msingi" imara wa kulinda TAIFA kama ilivyo sasa, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa za Chama kuwa ndio UTAIFA wenyewe.
Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi mkubwa hasa vijana ndio waathirika wakubwa.
Kwaundani zaidi, Bado haujachelewa, Pata Kitabu cha Ujasusi kwa Ofa ya Sikuu kwa @ 30,000/= badala ya Bei Halisi ya 80,000/= popote ulipo Tanzania.
Lipa 30,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.
Nje ya Dar utachangia nauli 8,000 tu