Naunga mkono hoja.............

Naunga mkono hoja.............

ChescoMatunda

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2009
Posts
1,232
Reaction score
442
Kwanza habari zenu wadau.
Tukaribishane japo kwa pilau.
weekend ndio hii msijenisahau
Leo Naunga mkono tuu hoja zenu.

Siungi uongo bali ukweli tupu
Wacha tule vyetu hatutaki -----
Usidhani nami nala malupulupu
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Watu walalama arusha na mtwara
Mbona hakuna amani au ni mkwara
Watu vipi tena mwarushiana mpira
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Kiranja kasema pigeni hao wakorofi
Hakuna maskhara hata kwa warafi
Wengine twajiuliza vipi sasa hawafi
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Kesi ya nyani na sokwe nani hakimu
Wewe mwanafunzi pia we mwalimu
Kufeli kwa mtihani nani tumlaumu
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Wengine wasema maisha magumu
Mzoee tuu hiyo hali halisi ngumu
Mjifunze kulisukuma gurudumu
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Hata ufumbuzi wa shida zenu
Nani wa kusikiliza vilio vyenu
Wakorofi waso hoja sio serikali yenu
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Maslahi yetu hayahusu msiosoma
Walalahoi chinga Nani kawatuma
Viherehere vyenu nasasa mtakoma
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.

Hata huruma sina nawe mvivu
Unalalama huku hutaki Kula mbivu
Mabadiliko hayataki uchovu uchovu
Leo naunga mkono tuu hoja zenu.
 
Back
Top Bottom