Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
Kuna watu mjadala ukiwa maadili yanavunjika wanawalaumu viongozi, na maadili yakinyooshwa wanawalaumu viongozi😃. Mara haki ya faragha, wengine hadi ushoga wameuweka kwa haki za binadamu.

Humu kuna anayependa dada yake ajiuzee? Kama jibu hapana, sasa tujadili kuwapa mitaji na pia tujadili kuwajenga kisaikolojia, lakini kuonesha anayewatoa kwenye madanguro kapora haki yao, hilo si sawa.


Tunajua madhambi yanafanyika, ila isiwe hadharani. Wale wako kando ya mashule, wanafunzi wanaulizana hawa wanafanya biashara gani? Wako Kando ya makazi ya watoto wanaokota kondomu.

Tutafakari.

====

Pia soma:

Kuna kesi ya udhalilishaji kama wale walioonekana kwenye video ya kukamata makahaba watapata mwanasheria mzuri

Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?
 
Wewe, unataka Lisuu,,fatuma na Sarungi wakumalize?
 
Inawezekana Watanzania ndio wanaongoza kwa Reasoning Capacity ndogo sana.

Watu wanapinga zoezi linavyoendeshwa kuingia na camera gesti kuwarusha watu kwenye vyombo vya habari madada poa na wanunuzi wa dada poa wakati mahakama haijathibitisha.

Mkienda Mahakamani ikathibitika baadhi hawana hatia na kwenye jamii mmeshawachafua, mtawasafisha vipi?

Kwanini hilo zoezi lisiendeshwe kwa kufuata misingi ya sheria?
 
Chukua hatua
 
Ujinga mtupu. Mnatusumbua tu

Unatetea kuwaondoa madada poa mtaani kwa makamera kisa maadili alafu unafunga mdomo kusemea maadili ya viongozi kujinunulia ma land cruiser LC300 karibu 400 nchi nzima kwa uchumi wetu? We unaona hayo ni maadili?
 
Kwanza neno maadili ni subjective

Kwa upande wangu kulipishwa tozo na kodi kandamizi ni ukiukwaji wa maadili.

Serikali inawaonea wivu wadada wawatu wanaojipatia kipato bila kulipa kodi.
 
Watengewe sehemu maalumu na walipe kodi - ile ni huduma ka ilivyo huduma nyinginezo. Walipe kodi - TRA anzeni kusanya kodi kwenye wigo huoo na watoe risiti 🤣 🤣
 
Wenye dada na mama zao makahaba hawawezi kukuelewa watakwambia uwaletee kifungu cha sheria
 
Anzisheni kwanza kampeni za kupambana na wala rushwa, wapigaji, na mafisadi kwa kuwarekodi na kamera huku mkiwa na magari ya polisi; muone kama hatutawaunga mkono.

Ila siyo kwenye haya mambo ya kipuuzi ya kutafuta kiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…