Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!


Pole sana mkuu kwa kwa kudakwa na pascal
 
ukiacha wananchi wa huko chato labda kufaidika kwao ni kupanda ndege nina uhakika hata wewe hadi muda huu hujawahi kuipanda hiyo ndege sasa sijui wa huko chato itakuwaje kwenye usafir ni punda

Eeeh
Nitumie nauli kabisa nipande ndege zikianza nikapatembelee Chato. Ila mmmh unanukia kama mia tisa itapendeza
 
Please Nirekebishe kwenye hili:

Je inawekana kuwa ni zaidi ya mwaka Sasa tangu mkuu aulizwe swali kwenye jumuiya?
Hahaha...mkuu, huyu jamaa alikuwa hajakutana na "real test" ya maswali ya waandishi katika wigo wa kimataifa. amezoea mikutano yake ya humu ndani ambako baadhi ya masswali huwa edited ili yasimkele bwana mkubwa...
 
Acha kukwepa ukweli mkuu Pascal!Hivi kweli kama ujenzi huo umepitia hatua zote za kuibua vipaumbele,kuvitengenezea sera,maamuzi ya ujenzi yakaamuliwa na mamlaka husika tena kwa uwazi hivi tungeshuhudia na kusikia kauli zinazosigana juu ya ujenzi huu?Au una-balance mambo?
 
Afu cha ajabu huyu mkuu anapenda sana kujinasibisha na kabila lake na kama ni hivyo why not kuendeleza Mwanza airport ambayo umuhimu wake upo dhahiri kiuchumi na kijamii, hii ingekuwa ni sawa tu na kuendeleza anapotoka maana sukumaland yote hiyo

Lkn kujenga li kitu kubwa kama hilo sehemu ambayo itachukua muda kuleta athari za kiuchumi na kijamii ni ku 'abuse' msemo wa mtu kwao

Angeiendeleza Mwanza airport inaleta maana sana hata hiyo credit ya kusema mtu kwao ingekuwa dhahiri sababu Mwanza ina athari ktk uchumi wetu kama Taifa na shughuli nyingi za ki biashara na kijamii zipo hapo pia ingekuwa ni 'hub' kwa ukanda huo

Huko kijijini angejenga uwanja mdogo tu tena kama wa dharura tu lakini kupanga ni kuchagua nasi muda mwingi tunachagua kwa mihemko
 

usifannaishe daraja la rufiji na ujenzi wa uwanja chato.
 
Ukisoma Alichoandika Pasco, na ukilinganisha Comments za baadhi ya watu humu, unajua kuwa bado Watz tuna safari ndefu sana, hivi vile vitabu vya fasihi andishi sijui havisomwi tena mashuleni? Haya mafacebook yamharibu sana vijana na watoto wetu.

Kiufupi Pasco anaichokonoa serikali ya awamu ya tano na kuna siku atakipata anachokitafuta.
 
Pascal umeshalemaa, post nyingi unaandika kwa mzunguko kama Shaaban Robert! Endelea kuwafundisha vijana namna ya kuandika satire. Asante kwa kutufunua macho kwamba kuna vitu vinaota kama uyoga huko Chato, miaka miwili tu tangu tumalize uchaguzi mkuu. Sasa tutajua kuvaa nguo nyeupe sio kuwa msafi.
 
Hawa watu ni wondersana Wameshindwa kuitengeneza airport ya zoo imechoka kwelikweli,,,chatokuna nini haswaa?

Ivi chato na Geita upi mkoa wenye watu wengi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…