Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!

Siku zote nayaheshimu mawazo yako na naheshimu kalamu yako Sana nikisoma tu na like.. Kwa hili hatuko pamoja.This is kind of genuine selfish na zambi yake itagharimu Taifa Kwa miaka mingi Sana .Kumbuka aina ya zambi hiyo alianza Samuel sitta kujenga ofisi ya Bunge kwao Kisa yeye spika.Mwisho wa Siku tutakua na maofisi Nchi nzima yasiyotumika Mungu tuepushe na laana hiyo ya umimi.Chato ilikuwa Bado kila jambo tuangalie economic impact
 
sijasoma content nzima. ila masahihisho kidogo. omukajunguti haiko bukoba. iko karagwe.
 
pascal uwe unawaonea huruma wanaojiita great thinkers lakini wana vichwa vya panzi wasioweza kusoma kati kati ya mistari.
 

Ggabolite ya Mabotu Sesse Seko au Yamasoukro ya, Félix Houphouët-Boigny....mbona humalizii mkuu, Chato ya JPM...!
 

Mkuu Pascal Mayalla hongera kwa hili bandiko ijapo ni la muda mrefu.
Hivi Mkuu Pascal Mayalla hili bandiko uliliandika ukiwa na furaha sana au hasira sana? Mkuu Pascal Mayalla kwavile bado naendelea kusoma mabandiko yako hapa JF, basi nina sababu ya kusema "Bwana asifiwe", "Tumsifu Yesu Kristo" au " Emmanuel".

Ahsante
 
Nchi ina hali mbaya sana! Hatutakiwi tuishi hivi, kwa nini tunafika huku, hadi mtu ashindwe kuongea mawazo yake kwa uhuru!?
 
Ugawaji wa Tausi huu Ugawaji wa Tausi, kabla ya Raisi Hajagawa tausi kwa wastaafu, kuna hotel inaitwa JS imeshapatiwa hao Tausi kitambo,

Ni mmiliki nani na nani hasa aliruhusu wato Ikulu?

Britannica
Mkuu Britanicca, acha uchokozi na uchochezi, tausi ni ndege tuu kama ndege wengine wote na wanapatikana mahali pengi.

Kwa bandiko hili, ikiamuliwa kufunguliwa kesi ya uchochezi, jee utaweza kuthibitisha kuwa hao tausi wa JS Hotel pale Chato ni tausi kutoka Ikulu yetu?, unamaanisha kuna mwizi kaingia Ikulu yetu, akawaiba wale tausi wa Nyerere pale Ikulu ambao ni nyara za taifa, akawapeleka huko JS hotel?.
Au anamaanisha miongoni mwa watu wenye access na Ikulu yetu, kuna mtu ni mwizi kaiba tausi wetu ambao ni nyara za serikali, na kuwauza kwa JS hotel ya Chato?.

This is criminal liability, hivyo kama kuna tausi wa nyara za serikali pale JS Hotel, Chato, na police wetu wanasoma JF, waanzishe uchunguzi hapo JS kuchunguza yafuatayo
  1. Jee ni kweli JS hotel ya Chato kuna tausi?.
  2. Waliwapata wapi hao tausi?
  3. Wana vibali vya kumiliki nyara za serikali?
  4. Kama ni tausi kutoka Ikulu yetu, nani aliruhusu nyara hizo za serikali kuchukuliwa na kupelekwa hotel binafsi?.
  5. Kama ni kweli tausi hao wa JS hotel ni kutoka Ikulu yetu, then huu nao ni ufisadi tuu kama ufisadi mwingine wowote!.
NB. Angalizo: Kufuatia proximity ya JS hotel kuwa karibu na Ikulu ya Chato, na the dividing line between JS hotel na Ikulu ya Chato ni very thin, na usikute tausi ambao Mkuu Britanicca amewaona hapo JS Hotel, akadhani ni tausi wa JS hotel , kumbe aliona kwa makengeza, due to parallax effects bila kuuona mpaka, tausi hao sio tausi wa JS Hotel bali ni tausi wa Ikulu ya Chato wakiranda randa hapo mitaa ya JS Hotel kama wale Tausi wa Ikulu ya Magogoni wanavyo randa randa maeneo mengi, and this being the case, hakuna kesi wala hakuna issue yoyote.
P
 
Kuna kitu najifunza kutoka kwa nguli Pascal....naamini.....historia inauwezo mkubwa wa kua upande wako...Kama nnachoamini ndo historia inachotaka.....Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…