Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!

Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!

very funny! katika watu wezi, wabinafsi, wenye wivu na ndumila kuwili...Magufuli ni baba lao. mkuu, unaonaje ukiomba kumfanyia interview Magufuli one on one? you know you're a journalist..na unaweza kuweka precedence ambayo waandishi wengine hawana tangia jamaa aingie madarakani@ Pascal Mayalla
 
Hahahaa Pasco you are so creative, kwa mtu mwenye mawenge hawezi kuona ujumbe uliomo hasa kwa wenzangu wa upande wa 'if you go slowly you can't cure the corruption disease', kwa uandishi wako I salute you.
Naunga Mkono hoja! Mkuu Pasco ana akili sana kwenye kujenga hoja zake na ubunifu wa kuukwepa mkono wa sheria pale inapobidi, kwa mtu wa kusoma mada zake bila tafakari hatoelewa na ataishia kumporomoshea mijitusi tu.
 
Kitu kilicho wazi na wazi kabisa, huyu hatatoka madarakani. Mobutu did all that shit knowing he is a president for life, hivyo anahitaji uwanja kwenda kwao inapohitajika na wakati mwingine wageni wa ndani na kimataifa kumkuta nyumbani ikibidi with ease of transport, which was justified, very justified kama atakuwa madarakani mpaka kifo! Huyu hatatoka madarakani! Huwezi kuwa unategemea kutoka madrakani miaka 10 tu ukafanya haya mabo ya matumizi ya fedha za serikali. Unfortunately enough watu wanamshangilia na wa tetemeko nshomile wahaya wanamshangilia! Nshomile kumbe bure. Pascal Mayalla
 
Wanabodi,

Tangu kupatikana kwa taarifa ya kutelekezwa kujengwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa eneo la Omukajunguti na badala yake uwanja wa kimataifa unajengwa Chato, kumetokea pingamizi kadhaa kupinga kujengwa kwa uwanja huo Chato kwa kutumia costs benefits index, hivyo mimi Naunga Mkono Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato, Una Justification, Utakuwa kama Ggabolite, au Yamoussoukro, Watalii Watamiminika kushuhudia miundombinu na kula raha Chato.

Justification why not Omukajunguti
imetolewa kuwa eneo hilo ni swamp area, ambayo ni very lame excuse, kama watu wanaweza kujenga hadi baharini kwa land reclamation, what is
swamp area kama mjenzi anajua anachokifanya ikiwemo kufanya elevation na kuweka vizuri water flows, watu waende Holland wakaone nchi iko under sea level, watu wamefanya land reclamation na wamejenga. Kinachotakiwa ni kujenga water flows tuu, hivyo argument ya swamp area doesn't hold water!. Ile hoja ya kuogopa kulipa fidia wageni, ni childish, assence ya fidia sio land bali ni development done on that land. Kama kuna mgeni mmemuacha hadi amejenga, then anastahili fidia. Hivyo hoja ya fidia nayo ni hoja tuu ya nguvu lakini haina nguvu ya hoja.

Justification Why Chato International Airport
Japo sijabahatika kuzisikia hoja kwa nini ni Chato International Airport, lakini mimi nimebahatika kufika Chato ile ya jamaa yangu fulani akiwa waziri, ndio alikuwa akimiliki the best hotel ya Chato ile. Kuna wakati nilikuwa na assignment ya mwezi mzima Biharamulo, lakini niliishi Chato, nikapanga kwenye hiyo the best hotel in Chato, ni hotel ya vijumba jumba vya detached suites.

Kama akiwa waziri tuu alishusha the best in Chato, sasa hivi alivyo, atashusha nini?.
Nimeteremka tena Chato na kiukweli Chato inabadilika kwa speed ya ajabu, vitu vinaota, na kuna kitu moja kimeshuka na kupanda juu, hii kitu sii kitu sii mchezo!. Sakafu tuu ni marble na granite, sofa za rooms ni pure leather, hadi WiFi Chato!, kwa mambo kama haya na kwa mwendo kama huu wajameni, uwanja wa kimataifa Chato ni halali na unastahili, kama haya tunayoyaona ni miaka mawili tuu, then kufikia miaka 10, Chato itakuwa an international city kama Ggabolite ya Mabotu Sesse Seko au Yamasoukro ya, Félix Houphouët-Boigny.

Utalii Sio Natural God Given Only, Hata Man Made.
Wengi wanadhani vivutio vya utalii ni natural God given only, sii wengi wanajua kuwa tourism attractions zinaweza kuwa man made kwa kujenga miundombinu ya kufa mtu ya kuvutia watalii, **** mji wa Sun City South Africa, au kuna mamia ya watalii wanamiminika kushuhudia a Catholic minor basilica dedicated to Our Lady of Peace in Yamoussoukro, the administrative capital of Côte d'Ivoire (Ivory Coast).

Kwa Nini Wanabeza Chato?.
Hivyo kuna wengi wanabeza uwanja wa Chato. kwa kijicho tuu cha wivu wa kwanini na sio wivu wa maendeleo, the real and true charity, begins at home, mimi naunga mkono 100% kwa 100%, kama umejaaliwa uwezo, anza kwanza kujenga kwako, ndipo ukajenge na kwa wengine!. Pia kuna uwezekano hata huu uwanja wa Chato, wanao beza ni wasiojua kutazama mbali, kwa sisi tuliofika Chato, na kuona vitu vinavyopanda, na hii ni miaka miwili tuu, then amini usiamini, baada ya miaka 10, watu watakuwa wanamiminika Chato, kuliko Mikumi!.

Naunga Mkono Uwanja wa Chato, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, Walifanya Makosa?.

Hivyo naunga mkono ujenzi wa uwanja wa Chato. Kiukweli Nyerere alifanya makosa kuhusu Butiama, Mwinyi akafanya makosa kuhusu kwao, Mkapa alifanya makosa kuhusu kwao, Kikwete amefanya makosa Msoga, Magufuli asifanye kabisa makosa Chato, miundombinu ya kuifikia Chato ikikamilika, kitu cha kuitumia miundombinu hiyo kitaibuka.

Chato oye!.
Mungu ibariki Tanzania.
Jumapili Njema.
Paskali
cc. britanicca
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pascal hayo madongo yako ni shida safi unamponda kwa code. Siku hiz kukuelewa inabid mtu atulie ndiyo ataelewa
 
Binafsi mimi siungi mkono hoja mwanza mwenyewe uwanja magumashi Kwa nn chato any way time Wil tell
 
Kuandika kwako kiujanja huchoki? Leo umechemka yaani umeonyesha huna hata fikra za kufikiria nje ya box... hata kufanya karisechi huwezi fikiria..unambeza tu..

Yaani na wewe ni kuwashwa washwa. nilitegemea utaongelea hata juu ya wananchi wa maeneo ya huko.. na jinsi watakavyofaidika katika mengi.. kuliko sasa wanavyotumia masaa mengi kufikia uwanja wa ndege wa karibu.

Leo umechemka na wewe umekuwa mdaku mwenye wivu ulivyombeza Mkulu tena.

Pole yako kumbe hauna maujuzi kabisa zaidi ya udaku.. ngoja nikuchekeeee ha ha haaaaa
 
Wengi waliotembea nchi za wenzetu hasa zilizoendelea, kuwa na ka Airport kama Chato sio mbaya, uwanja wa ndege sehemu yoyote ile ni muhimu hasa katika kukuza uchumi, labda iwe sababu kwanini Chato na sio Pemba au la, dola ijitahidi sehemu kama Chato ziwe na Airport..
Tatizo hapa ni sababu ndipo Rais wetu atokapo, zaidi ya hapo wengine tunaona poa tu..
 
Mkuu Paschal na wewe siku zingine sijui huwa unatumia kinywaji gani jioni? Mwanza kwenyewe hawana uwanja wa ndege, Mkulu akimaliza muda wake nani atakuwa anaenda Chattle?
Wakati mwingine tumia hata robo ya ubongo wako kujaribu kuelewa habari iliyoandikwa!
 
Mkuu Paschal na wewe siku zingine sijui huwa unatumia kinywaji gani jioni? Mwanza kwenyewe hawana uwanja wa ndege, Mkulu akimaliza muda wake nani atakuwa anaenda Chattle?
vijana hampendi kusoma na kuelewa ndio mana mnacomment kitotot hivi
 
Back
Top Bottom