Naunga timu kupewa Manji

Mgagaa na Upwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
13,481
Reaction score
28,116
Yanga inabadilishiwa mfumo wa umiliki na uendeshwaji tu sio kuuzwa au kukodishwa . Mfumo uliopo ni wanachama kupitia uongozi waliouchagua kuimiliki na kuiendesha klabu kwa asilimia 100.

Sasa inakwenda kumilikiwa na mtu mmoja kwa asilimia 75 na 25 zikibaki kwa wanachama .

Mkataba husika kuendeshwa kwa miaka 10 ni sawa na ubinafsishwaji wa sehemu ya umiliki ili klabu ijiendeshe kwa faida kama yalivyofanyiwa mashirika ya Umma mwanzoni mwa miaka ya 90.

Kilichopo ni kuhakikisha " Brand " ya klabu inakua kwa haraka na faida kwa mwekezaji husika na klabu.

Miaka 81 hakuna la maana hata Azam FC yenye miaka 8 chini ya mtu mmoja inajeuri ya kuongea sasa tuache hii miaka 10 tuone nini kitafanyika .

Watu wanasema atapata faida kubwa sana na sisi kuendelea kubaki masikini . Kwa miaka 10 ametoa pesa sh ngapi ambazo hazijampa faida yoyote zaidi ya umaarufu?!

Tulipofikia hata kumuuzia ingewezekana poa tu maana walibaki wachache wananufaika timu inazidi kuwa masikini bila maendeleo yoyote.

 
vipi hayo mashirika ya umma baada ya kubinafsisha nin kilitokea?
 
Manji kama Magufuli anatumbua majipu ad kwenye club..

Hatujauza tumekodisha na hatujamkodisha hiv hiv tumeona vision yake na wapi tunaenda ndio maana imekua rahisi kwetu kiroho swaaf..
VivaManji
Daimba Mbele Nyuma Mwiko
 
Hata haya mafanikio tunayo jivunia yametokana na mchango wake mkubwa ila wengi wetu kupinga ni jadi.
 
Mkuu nimekuelewa kwenye huo mfano wako wa Azam fc, ila kuna haya maswali hapa unaonaje ukatusaidia kuyajibu kwa maana ni kama unajua nini kinachoendelea huko ila pengine sisi wengine hatujui. Hebu ingia uzi huu hapa ukatujibie maswali yetu au yeyote anayejua atusaidie.
Kufuati tetesi za Manji kukodishwa timu, tunaomba majibu ya maswali haya.
 
Nyie wote mshakula ela yake sasa mnavimbirwa vibaya ata mtoto mdogo anashangaa timu kukodishwa tena ata bila kuonesha ni shngap
 
Hatua zozote zinachokuliwa na MANJI ni MWIBA kwa MAKOMANDOO na wale wote walioiishi muda mrefu kwa Kuitegemea Yanga, ikumbukwe kuna WATU(Wanachama) wameelimisha Watoto (Shule) kwa mgongo wa Yanga,kuna baadhi wamejenga Nyumba kupitia Yanga,kuna watu Wanamiliki magari mazuri tu kwa jasho la Yanga,....Leo hii walio mstari wa mbele kuhoji hatua zozote ambazo Manji anafanya kwanza mchunguze,Je ni kweli ana wanachungu kweli na Yanga ? wanachangia kiasi gani maendeleo ya Yanga,? Lini alitengeneza Proposal yoyote juu ya namna gani Yanga ifanye iliisonge mbele? Jiulize hizi Page za Facebook,Twitter,au mawasiliano kwenye Instagram,Whattsapp,zinaweza kweli kufikisha mchango(mawazo) kwa Uongozi wa Yanga hasa mwenyekiti Yusuf Manji? au staili hii ni mbinu za kupayuka ili Mwenyekiti akuiite akuambie acha kupayuka na bahasha mkononi?, Hivi kuikodisha NEMBO ya Yanga na kubaki na Makomandoo wanaoitafufana klabu lipi lenye faida ?,.Kuendesha mpira zama hizi ni gharama, hiki siyo kile kipindi cha kusajili mchezaji kwa mapenzi ya klabu,ukifanya hivyo utaiishia kupata wachezaji wa kiwango cha chini na hatimaye timu inafanya vibaya na kushuka daraja,fahari itabaki Majengo kama walivyo PAN AFRICA.
 
Kuna watu hawajawahi kuchangia Yanga hata sh.mia. leo wanajifanya wana uchungu sana na Yanga
 
Katika kikao walichokaa cha Kuikodisha Timu ya Yanga kwa Mkodishaji kati ya wateja wanaotaka kukodishwa Yanga na Wenye timu ya Yang a , Mtu mmoja aitwae Manji alihudhuria kikao hicho kama Mkodishwaji Mkuu (Tenant) na pia mtu huyohuyo alihudhuria hicho kikao kama Mkodishaji Mkuu(Landlords).


Akiwa kama Mkodshwaji Mkuu (Tenant), Mtu huyo aliweka terms za mkataba anaoutaka (proporsals) yeye mteja ambao alidhani kama Mkodishwaji Mfanyabiashara angefaidika nao, lakini Mtu huyohuyo mmoja akiwa kama Mkodishaji Mkuu (mwenyemali) ambae alitakiwa kufikiri kwa faida ya wenye mali wenzie alikubaliana na terms/proporsal zilizowekwa na mteja ambae nae ndio yeye yeye mwenyewe!!

Yaani katika Meza ya majadiliano iliyohusisha pande mbili za Landlord v/s Tenant, mtu huyo ikifika zamu ya Landrod kuongea basi anahamia upande wa Yanga na anaanza kuongea kama mwenyekiti na anatoa hoja, na ikifika zamu ya tenants kuongea basi nae ananyanyuka kwenye kiti na kuhamia upande waliko wafanyabiashara wenzake anaongea kama tenants Mkuu akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa mwenyekiti ambae ni yeye mwenyewe.

Na wakifikia makubaliano basi katika Mkataba mtu huyohuyo anasaini sehemu ya Landlord na anasini sehemu ya Tenants. Yaani Mwenyemali Mkuu ni yeye, na mteja Mkuu ni yeye pia,
 
Umesema kweli mkuu... Lakini acha tumpe timu tu, hakuna namna
 
Ilimradi tu waonekane wanapinga si unajua hapa Tz sahivi kupinga ni kipaji na kila mtu anatamani awe nzcho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…