Nauona Upinzani Ukiichukua Nchi 2030

Umemaliza kila kitu. Muda utasema!
 
Uchambuzi sahihi, unaona ninachokiona.
 
Ni mtazamo mzuri, ila please lets share, kati ya hive vyama 18 vya
Siasa, ni chama gani hicho cha kushika dola 2030?.

Hata mimi niliwahi kuwaza kama wewe Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
 
Umeandika mambo mengi kama vile hivyo vyama vya upinzani vipo.Watanzania wameshakatishwa tamaa na maswala ya kisiasa kiasi kwamba wameachiwa kajikundi kadogo chenye fedha kushika hatamu yote ya nchi wewe ukileta fyoko utaokotwa ununio.Hakuna namna yoyote ya Watanzania kunasuka ktk makucha ya hawa watu. Kwa sasa na wanazidi kujiimarisha.Kwa mfano uchaguzi wa mwaka huu vyama 18 vinashiriki uchaguzi vyote vyama vya upinzani ni dhoofu hali wagombea wake wanahali ngumu kupita kiasi na asilimia kubwa ni mapandikizi.Tunakwenda kuiteketeza nchi kabisa kama watu wenye ushawishi mkubwa kwenye nchi hii wasipo chukua hatua nakulithibiti hili janga la mwaka huu tunakwenda kutumbukia kwenye giza nene sana nakutoka huko itakuwa kazi sana.Tanzania inakwenda kua Mradi wa watu wachache na Wananchi wanakwenda kupokwa kila kitu.Kuanzia ,mahakama ,bunge na serikali kuu.Sidhani hata hii jamii forum itakuwepo awamu inayokuja.itakuwa giza giza totoro.kwa sababu wahusika watakuwa wamejiimarisha nyanja zote.Wala Mama hana Tatizo Lolote Tatizo lipo kwa Wabara.Ni mshauri Mama Ajitahidi angalau kwa asilimia 30 awapatie Watanzania katiba mpya.
 
Hata mkalale bila nguo kwenye kaburi la baba wa taifa, hamchukui nchi
Muda wenu wa traditionalists, Baby Boomers na Gen X unaelekea ukingoni, na hapo ndipo Millennials, Gen Z na Gen A watakapofanya mabadiliko (point no.3 kwenye short terms). Na pia kama umesoma vizuri nimesema hata upinzani kuichukua nchi inatakiwa na yenyewe ije na strategy za maana (soma closing remark)​
 
Nakubaliana nawe kuwa udhaifu wa vyama vya upinzani na hali ya wananchi kukata tamaa ni changamoto kubwa sana. Ndiyo maana katika hitimisho langu nilisisitiza kwamba nafasi ya upinzani siyo cheque wazi. Bila mshikamano, uthubutu na ajenda za maana zinazogusa maisha ya wananchi, 2030 inaweza kubaki ndoto ya kufikirika tu.

Hata hivyo, historia imeonyesha mara nyingi kwamba hata pale ambapo mfumo unaonekana kujiimarisha kupita kiasi, mabadiliko bado hutokea kupitia mwamko mpya wa wananchi, vijana, au hata baadhi ya watu waliomo ndani ya mfumo huo. Kwa hiyo, ni kweli changamoto ni nzito, lakini siamini kuwa tupo gizani kabisa bali tupo katika njia panda.​
 
Asante ndugu yangu kwa kunikumbusha uzi wako wa 2018 na kwa kweli ulikuwa na hoja nzito sana. Swali lako ni muhimu: ni chama gani kati ya hivi 18 kitaweza kushika dola 2030? Ukweli ni kwamba kwa hali tuliyonayo sasa, bado hakuna chama kinachoonesha wazi uwezo wa kushindana na CCM kitaifa.

Lakini kama ulivyowahi kusema, 2030 inaweza kuwa mwanzo wa mwisho si kwa sababu chama kimoja kitakuwa tayari kimejijenga, bali kwa sababu mazingira ya kijamii, kiuchumi na kizazi kipya cha wapiga kura yatakuwa yamebadilika. Kwa maneno mengine, 2030 huenda isiwe ushindi wa chama fulani, bali ushindi wa mazingira mapya yatakayolazimisha mfumo wa siasa kubadilika.

Kwa sasa hakuna chama cha kutaja moja kwa moja, ila tunaweza kusema kwamba yeyote atakayeshika dola 2030, hatakuwa na nafasi bila katiba mpya, tume huru na mshikamano wa upinzani.​
 
Hakuna mwamko wowote wa vijana wa nchi hii asilimia kubwa ya vijana wa Tz hawana Elimu na ndiyo hao wanaotumika wale ambao wamesoma wengi wao ni waoga kupita kiasi.Niseme tu tukubaliane na hali ilivyo kama unakashughuli kako kaghagh'anie tu basi ili usife njaa
 
Hii ni kauli ya kukata tamaa ndugu yangu, kama upo mtaani utakubaliana na mimi kwamba wimbi kubwa la vijana (wasomi na wasio wasomi) hawaitaji hata kuisikia sisiemu, mfano mzuri angalia namna wananchi (Yanga) walivyoishambulia team yao baada ya kuichangia sisiemu pale M City​
 
Bado unaamini hili la uoga lipo kama ulivyokuwa unadhani? Bado ccm inajiaminisha itaendelea kukaa madarakani kwakuwa vijana ni waoga kupita kiasi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…