Nauona ushindi wa Taifa Stars hapo kesho lakini Kamati ya Ushindi ina ukakasi. Kesho tunaandika historia mpya!

Nauona ushindi wa Taifa Stars hapo kesho lakini Kamati ya Ushindi ina ukakasi. Kesho tunaandika historia mpya!

Mungu wetu ni mwema sana. Ameiongoza na kuilinda timu yetu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) hadi ilipofikia. Aneipa alama ilizonazo sasa na kesho anaipa nafasi na baraka za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika. Kesho ni siku yetu.

Uwepo wa wachezaji wetu wanaocheza nje na ndani ya Tanzania kupambana na majirani zetu Uganda ni kiashiria tosha cha kufuzu kwetu na kuandika historia mpya ambayo itakumbushia kufuzu kwetu mwaka 1980,mwaka ambao sina hakika kama kuna mchezaji yeyote atakayecheza kesho alizaliwa. Nauona ushindi wetu kesho.

Imeundwa Kamati ya Kuhamasisha ushindi wetu hapo kesho. Kwakuwa mimi si rafiki wa unafiki,nauona ukakasi wa wazi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Paul Makonda,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kamati imejumuisha watu maarufu tu ambao hata danadana mbili hawajawahi kupiga.

Kamati ya Makonda inapoteza lengo. Ushindi wa timu huanzia kwa wachezaji na si watazamaji au mashabiki. Kutingwa na watazamaji na mashabiki badala ya wachezaji ni kupoteza uelekeo. Kesho unachezwa mpira. Mpira si kama siasa inayotegemea porojo,propaganda na utapeli. Soka ni muunganiko wa uwezo wa wachezaji na saikolojia yao.

Naamini Tanzania ina wachezaji wenye vipaji. Kati yao wanaunda timu ya Taifa. Kinachopungua miaka yote ni kukosekana kwa saikolojia ya kujiamini,kupambana kwa ajili ya taiga letu,kujitoa na kuwa makini kwa kila sekunde ya mchezo. Kamati ya Makonda ilipaswa kujielekeza huku.

Kamati ilipaswa kujumuisha baadhi ya mashujaa wetu wa 1980 walio hai ili kuwaaminisha watoto wao wanaocheza kesho kuwa kila jambo linawezekana. Wapi akina 'Computer'? Anaingiaje Haji Manara akaachwa Sunday Manara baba yake na mmoja wa mashujaa wa 1980? Isigeuzwe ni Kamati ya sherehe kabla ya ushindi!
Tulizembea kwenye mech ya kufuzu huko kwa king mswati ko kipigo kinatuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza namshukuru alie juu MWENYEZI MUNGU kwa kuniwezesha kuandika uzi huu. Yaa rabbi nakuomba mechi ya kesho tufungwe nyingi ili mara nyingne tujue kuwekeza katika mpira. Ilikua tufuzu mechi iloyopita tukafanya madudu kocha akajaza mabeki badala ya kujaza viungo ili mpira unoge hatimae tukafungwa saivi tunaomba njaa kwa wenzetu wafungwe yaa rabbi tunakuomba tufungwe akili itukae vizur sifa zimezidi.
WABILLAH TAWFIQ

Sent using Jamii Forums mobile app
Tufungwe tuuuuuuu
Ikishinda sifa zitapelekwa kwa JIWE
 
Nyi mmepotoshwa na kina Bashite sio kama kesho Tanzania ikishinda ndio imefuzu hiyo nafasi moja inagombaniwa na
LESOTHO
CAP VARDE
TANZANIA
Ili Tanzania ifuzu inabidi tumfunge Uganda na Cap varde amfunge Lesotho sasa huyo Mungu wetu peke yetu
Mechi yetu ya kufuzu ni ile ya mwisho tulio ipoteza laki hapa tunadanganyana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa 0 uganda 5
IMG-20190323-WA0036.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaliyopita si ndwele, tuungane kuiombea timu yetu ishinde na kufuzu ingawa yule kocha ni kweli ana maamuzi ya hovyo hovyo yasiyotabirika.
 
Nyi mmepotoshwa na kina Bashite sio kama kesho Tanzania ikishinda ndio imefuzu hiyo nafasi moja inagombaniwa na
LESOTHO
CAP VARDE
TANZANIA
Ili Tanzania ifuzu inabidi tumfunge Uganda na Cap varde amfunge Lesotho sasa huyo Mungu wetu peke yetu
Mechi yetu ya kufuzu ni ile ya mwisho tulio ipoteza laki hapa tunadanganyana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wao wanachofahamu kuwa Taifa star ikishinda watauziwa balimi kwa sh.500/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nilishasema hii nchi ina wajinga wengi mno ndo maana ipo hivi ilivyo. Mpira hauhitaji maombi..hata huyo Mungu(kama yupo) atakuwa wa ajabu,yaani aache kushughulika na wagonjwa na wenye uhitaji ashughulikie burudani!??

Halafu watu ni wajinga kwelikweli,hata akili za kawaida tu mnakosa,huyo Mungu si atakuwa kibarua wenu!?? Yaani mumuombe awasaidie muifunge Uganda,halafu wakati huohuo muombe Lesotho afungwe au atoe sare. Huyo Mungu si bora ahamie Tanzania tu...!! Mpira unachezwa hadharani bhaana,hakuna cha maombi hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom