Nautamani ule mtaa wao

Nautamani ule mtaa wao

philosophy

Senior Member
Joined
Nov 11, 2012
Posts
104
Reaction score
42
NAUTAMANI ULE MTAA WAO
Wakati anakuwepo, alikuwa ni yeye pekee aliyehitaji kuwa kama anavyotaka kuwa. Aliufikia uwezo wake wa kimaumbile aliojaliwa, na kujitambua kuwa yampasa autumie vema ili aweze kumudu maisha yake. Katika ndoto zake yeye alikutana na kiumbe kama yeye ijapo yule kiumbe mwenza alikuwa ni jinsia kinyume chake. Hakika, nusu ikungana na nusu, basi kizima kinakuwa. Yeye ni uwepo, akakutana na uwepo mwingine; ndipo, uwepo kamili ukatimia kwa nguvu ya msukumo wa kimaumbile. Kwa kuwa alikuwa na tajiriba hizo, aliutambua ukweli hakika ambao kuuishi ni kudhihirisha utu. Alijua kuwa uwepo bila utambuzi nafsia hauna maana yoyote. Ndipo kwa kuwa walikuwa ni wawili, yeye aliogopa kuwa msaliti wa nafsi yake, kwa kumpatia ubavu wake wa kushoto elimu ulimwengu ambayo pasi shaka ilimjengea msimamo bora wa kuwa mtu aliyekuwa kamilifu. Elimu hiyo, yeye iliufanya ubavuwe wa kushoto kuwa mwanadamu anayestahili, aliyejua wajibu wake na kuutimiza vema. Alikijua chanzo chake na kutambua zawadi aliyonayo ya urazini amabayo humtofautisha na wanyama wengine. Kwa msingi huo, maumbile-dunia yaliwafanya wote wawili watambue kuwa kupitia fikara zao mantiki, wao wanayo nafasi pekee ya kuibadili dunia yao chini ya utimizaji wa wajibu wao kwa kile kilicho chini ya uwezo wao. Hata pale walipofanikiwa kuwapata viumbe wao wengine (watoto), hakika waliwalea kama wao wenyewe walivyoishi na kukuzwa kwa kuwapa miongozo na misingi imara iliyojengeka chini ya elimu-fikara-ukombozi. Misingi hiyo, kwani, ndio iliyokuwa mwanga-angavu wa maisha ya familia yao kwa sababu tu ilimfanya kila kiumbe ndani ya fanilia ile kuishi kama mtu apasavyo kuwa. Waliyaona na kuyaishi maadili; busara ilikuwa ni mwaongozo wao; elimu iliwafanya hata wao pia kuona kuwa wao ni watu wanaostahili usifa huo. Ilikuwa ni familia bora iliyojengwa na kufuata misingi ya kiini cha utu. Kila raia katika mtaa ule aliuone ukweli hakika wa maisha yao na kuvutika kuwa kama wao. Kama ilivyokuwa kaida ya msukumo wao wa ndani, ule wa kuutafuta ukamilifu wa utu; hakika, hawakusita kutimiza jukumu hilo la kuukomboa mtaa wao. Walifanya hivyo, miaka hadi miaka, hatimaye wakafanikiwa mbegu bora za utu ndani ya mioyo ya wanamtaa wenzao. Nao ukombozi ulitimia. Hili ni jambo ambalo lilifanikisha kuwatoa wanamtaa ule katika maisha ya “astiria ya pango” na wao kuona mwanga wa jua kwa mboni-aksi za macho yao, ijapo jua hilo lilikuwa kali sana kwa kuchoma uso wao na kwa kiasi ilisaabisha madhara katika miili yao ila kwa baadaye majeraha hayo yaliwapona. Ukombozi huo japo ulikuwa shubiri kwa kiasi, lakini ulifaulu kwa mwendo wa ajabu sana kuleta matunda ya kuufanya mtaa ule uwe na wakazi ambao ni watu na wala sio biandamu tu. Kila kilichofanywa kwa muda huo kilikuwa chini ya mwangaza angavu wa upendo, busara,hekima, uelewa wa hali ya juu sana; jambo ambalo lilijenga ngome ya haki katika kila nafsi ya mtu. Roho zao zilifarijika na kufurahia maisha murua chini ya uongozi wenye fikara mantiki ambazo zilijengwa na mwangaza wa umaarifa – ongozi ambao msingi wake ulikuwa ni yeye aliyefunza umma wake utu. Hakika, nautamani ule mtaa japo msimulizi alikata pumzi kabla hajamaliza simulizi yake.
 
Back
Top Bottom