Nauza hatimiliki ya tamthiliya

Nauza hatimiliki ya tamthiliya

Sokoro waito

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
2,201
Reaction score
2,599
Habari ndugu zangu? Mimi ni mwandishi wa vitabu vya tamthiliya na mashairi. Kitabu cha Tamthiliya hii ninayoiuza chaweza tumika kwa mambo yafuatayo: 1.kutengenezea filamu nzuri kwa biashara. 2.kuiandika kwenye magazeti na kuiuza kama hadithi kwa wasomaji, hii itapelekea wasomaji kuifatilia na kuendelea kununua gazeti husika. 3.kusomwa kama kitabu cha ziada au kiada kwenye shule za sekondari au zaidi, na hivyo chapa nyingi kuhitajika ambapo mmiliki atanufaika kwa kuuza hizo chapa. 4. Kwenye blogs zinazouza machapisho kupitia njia ya mtandao. Asilimia 5 ya mauzo atapewa mleta mteja mnunuaji. Tuwasiliane kwa PM or Private message kwa yeyote awezaye kununua au kuniunganisha na wanunuzi. BEI NI MAELEWANO.
 
Hongera, kasajili haki yako ndo uanze kutafuta wateja, wapigaji wapo wengi kaka
 
Habari Tanzania? Mimi ni mwandishi wa vitabu vya tamthiliya na mashairi. Nauza kitabu cha tamthiliya ambacho chaweza kutumika kwa mambo yafuatayo: 1.kutengenezea filamu kwa biashara. 2.kutumika shuleni kama kitabu cha kiada na ziada wakati serikali itakaporuhusu hivyo, hii itampelekea mmiliki kuuza chapa nyingi na kupata kipato. 3.kuuzwa kwa kuchapwa kwenye magazeti kama hadithi ili kuvutia wasomaji. 4. Kutumika kwenye blogs zinazouza machapisho kwa njia ya mtandao. BEI NI MAELEWANO KULINGANA NA MATUMIZI YAKO. Tafadhali msaada wenu wanajamii nipate kuuza hii mali.
 
Hongera kwa hilo. Bila shaka wadau watafanikisha lengo
 
Sokoro waito

Ndugu, naomba elimu kidogo na majibu ya maswali machache

1 - Naomba unikumbushe nini maana ya tamthilia?

2 - Tamthilia zako walengwa wako ni wa umri gani?

3 - Je Tamthilia zako zina picha? <Kama ndio, mchoraji nani?>

4 - Zaidi ya tamthilia na mashairi, je una ujuzi mwingine kama utungaji wa vichekesho? (Kama ilivyokuwa Sani?)

5 - Kwa sasa una tamthila ngapi?

6 - Je una tamthilia yeyote ambayo imeshatumika kutengeneza filamu au ina kitabu?

7 - Kama una kitabu, je ume-apply serikalini ili ki/vitumike mashuleni?

Nafikiri majibu kwa haya maswali yanaweza kusaidia wadau wengine ambao wana interest kama mimi. Pia naweza kuwa na maswali mengine in private or public.

Asante.
 
Last edited by a moderator:

1.Tamthiliya ni simulizi yenye maudhui mbalimbali kwa jamii husika, yaweza kuwasilishwa kwa njia ya luninga(kama filamu),magazeti(kwa maandishi kama hadithi) radio(kama maigizo ya sauti) n.k 2.walengwa wangu ni wa umri kuanzia miaka 13 na kuendelea hadi wazee. 3.tamthiliya yangu haina picha. 4.nina ujuzi wa kuweza kuandika vichekesho vya katuni,mashairi,nyimbo za injili na kuimba pia. 5.nina tamthiliya(kitabu) moja iliyo tayari na kitabu kidogo cha mashairi. 6.hapana sina tamthiliya iliyoigiza filamu. 7.sijawahi kuomba kitabu changu kuruhusiwa kutumika shuleni. Kwa maswali zaidi naomba uniPM or Private message ili tupeane contacts. Asante.
 
Last edited by a moderator:
Naomba niendelee kuuliza hapa kwanza ili jamii yote iweze kunufaika kwa mtu yeyote mwenye maswali kama yangu. Hii itakusaidia wewe pia kutokujibu swali moja zaidi ya mara moja. Kuna maswali mengine yatakuja private.

1 - Kwa hiyo ni hadithi za kufikirika? < Kama ilivyokuwa Mama na Mwana? >

2 - Je kitabu kilicho tayari kina sura ngapi? Na kinaweza kutoa kurasa ngapi?

3 - Je kazi ya uandishi / utunzi umeanza lini?

4 - Je una kazi yoyote ambayo umesha-publish kwenye public domain?

Hope to hear from you again.
 
asante kwa maswali mazuri 1.Hadithi hii sio ya kufikirika kwa ujumla ila kuna maeneo machache niliweka maneno ya kufikirika. 2.kitabu kina sura 5 na kurasa 60 3.Kazi ya uandishi nilianza mwaka 2010. 4. Sina kazi yoyote nliyopublish kwenye public, japo mwaka 2012 nilipoandika kitabu kidogo cha mashairi nilitafuta sana kampuni ya kunisaidia kureview na kuprint hicho kitabu, nikapata kampuni ya Dorance publishing company ya United states ambao walikubali kureview kazi hiyo kisha wakanijibu kuwa kazi ni nzuri, hivyo tuendelee na printing iliyotakiwa niwalipe dollar 2000, kwa gharama za marketing,distribution and sales tulikubaliana wakate asilimia 25 kwa kila copy ambayo wangeiuza kwa muda wa miaka 5 kisha wangenirudishia copy zilizobaki. LAKINI PESA YA PRINTING AND PUBLISHING ILINIKOSA HIVYO HII DEAL IKANIPITA!!! ILINIUMA SANA MAANA HATA TZ COs' nilizoomba ilishindikana. Kwa kuwa nlikuwa chuo kusoma nliamua kuconcentrate zaidi kwenye masomo zaidi ya uandishi. KARIBU KWA MASWALI ZAIDI.
 
Back
Top Bottom