Hiyo elfu 50 kwa mwaka ni dividend na haina uhakika, inawezekana mwaka unaofuata ikaongezeka au kupungua. Cha msingi zaidi angalia capital gain; hisa uliinunua sh. ngapi na sasa ina thamani gani. Halafu angalia matarajio, je kampuni inaelekea kukua au kufa? Kwa NMB ningekushauri ukae nazo hisa zako kwa sababu kampuni bado haijafikia plateau.
Kipindi hiki cha sikukuu watu wengi huuza hisa zao. Inadhaniwa kuwa wengi hufanya hivyo kwa malengo ya kupata pesa ya sherehe, kwa hiyo jifanyie self analysis kama kweli unataka kufanya business nyingine au umekuwa caught up kwenye mood ya kula good time mwisho wa mwaka.