Nauza hisa za NMB

Nauza hisa za NMB

Kachoki

Member
Joined
Feb 2, 2010
Posts
29
Reaction score
4
Wapendwa nauza hisa za NMB ushauri jamani niziuze au niziache lakini hisa zenyewe elfu moja tu gawio kwa mwaka elfu hamsini lipi bora kuziuza kufanya shughuli nyingine au

Ulizinunua pesa ngapi?
 
Wapendwa nauza hisa za NMB ushauri jamani niziuze au niziache lakini hisa zenyewe elfu moja tu gawio kwa mwaka elfu hamsini lipi bora kuziuza kufanya shughuli nyingine au

Kachoki

Elfu 50 kwa mwaka mkuu hata ukifanya biashara ya genge hiyo elfu 50 utapata kwa wiki so tafuta profitable bss na uuze hizo hisa uziweke hapo utamake hela mkaka mwenyewe utajuta kwanini ulishikilia hizo hisa
 
Elfu50 kwa mwaka!!
Yaani ni sawa na kupata sh 4,166 kwa mwezi, ambayo ni sawa na sh 137 kwa siku.
Yataka moyo sana.
 
thamani ya hisa zako ni ipi?
hebu kuwa muwazi
twaweza nunua hizo hisa
 
Hiyo elfu 50 kwa mwaka ni dividend na haina uhakika, inawezekana mwaka unaofuata ikaongezeka au kupungua. Cha msingi zaidi angalia capital gain; hisa uliinunua sh. ngapi na sasa ina thamani gani. Halafu angalia matarajio, je kampuni inaelekea kukua au kufa? Kwa NMB ningekushauri ukae nazo hisa zako kwa sababu kampuni bado haijafikia plateau.
Kipindi hiki cha sikukuu watu wengi huuza hisa zao. Inadhaniwa kuwa wengi hufanya hivyo kwa malengo ya kupata pesa ya sherehe, kwa hiyo jifanyie self analysis kama kweli unataka kufanya business nyingine au umekuwa caught up kwenye mood ya kula good time mwisho wa mwaka.
 
Nakushukuru kwa ushauri nitafanya self analysis then niamue lakini si kula good time ila nilikuwa naangalia ni bora nikazizungusha maana zimekaa huko miaka miwili sasa lakini sioni faida
 
Back
Top Bottom