Plot4Sale Nauza kiwanja kwa Tsh. Milioni 3

Kutoka Morogoro mjini hadi mkundi nauli ya daladala ni shs 700 na distance Ni 12Km kutokea pale Msamvu,Mkundi ipo Dodoma road
Details za kutosha na kama ni surveyed plot utapata mteja soon naomba unipm mkuu...
 
Kama alikuwa ana mpango wa kununua atakinunua. Kama hakuwa na mpango huo basi amemsaidia mnunuzi atakayekinunua....

Kila la kheri mkuu. Ningekuwa Moro yani leo kabla saa sita mchana ungepokea simu yangu....
 
Hii ni makunganya hii! Umbali kutoka kiwanja na barabara ukoje?
 
Nilisitisha zoezi Mkuu, nilitatua changamoto yangu
Halafu nyinyi watu wa Morogoro sijui mna shida gani! Kuna mwenzako naye aliwahi kuleta tangazo humu jukwaani, la kuuza kiwanja chenye ukubwa wa nusu heka maeneo ya Kihonda.

Siku nimejichanga, nampigia tufanye biashara! Akanipa jibu kama hili la kwako. Kiufupi alinikera sana.
 
Tate iwe,punguza kulaumu Mkuu,mtu hadi akiamua kuuza asset yake ujue kuna dharura imemfika,hutokea akapata suluhu ama ahueni wa Jambo linalomkabili na akabadili maamuzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…