30X50m? au 30miguu x 50miguu?..maana kwa uelewa wangu wa viwanja hasa maeneo uliyoyataja huwa hawapimi mita wanatumia miguu na mbaya zaidi huwa ni miguu ya muuzaji ambaye anatembea taratibu hatua ndogondogo ili shamba lake atoe viwanja 50 apate pesa nyingi...
please cofirm kama ni kipimo cha mita ili nianze kukushusha bei maana najuwa watu kibao watazichomolea hizo slopes za huko na huo udongo mfinyanzi wengu tunaufahamu kwa kupasua misingi ya nyumba...kama ni miguu wala sihitaji kuongea zaidi nakuwa nimeishajitoa katika list ya wateja wako watarajiwa
Mkubwa nieleweshe kidogo hapo 30x50 sijaelewa ukubwa wake vizuri je imefika eka moja??Mimi nina kiwanja changu hiyo hiyo barabara kule karibu yanapoishia yale magari ya usafari I mean pale karibu na shule sasa sijui wewe!!
yaani JIRANI unataka kumuamisha mwenzako???duhhhhhhhhhhh
...Nadhani ni zaidi kidogo ya NUSU eka kama tutakubaliana na vipimo vya wanaouza mashamba maeneo hayo kuwa Ekari moja ni maguu 70x70. Nisahihisheni.
Haya mahesabu ya maumbo yalikuwa yananipa taabu kweli. Kwa sababu kama 70 x 70 ni hekari 1, sijui 35 x 70 zitakuwa hekari ngapi, hasa ukitilia maanani kuwa 30 x 50 ni zaidi kidogo ya nusu heka!
lol
Mwanzoni hili swala la miguu lilikuwa linanichanganya kiaina. Na mara nyingi mtu akisema 30 x 50 anamaanisha miguu, ingawa ni vizuri kuuliza.
Eka moja ni mita za mraba 4,046.85642.
Kwa hiyo eka moja ni 63.6m x 63.6m .
Waliposema hiyo ni sawa na 70miguu x 70miguu, walimaanisha miguu 70 ni sawa na meter 63.6 . Yaani mguu mmoja ni 0.9m (90cm). Kwa watu wenye urefu wa kawaida, ukijaribu kupiga hatua zenye urefu huo wa 90cm, utagundua kwamba ni hatua kubwa kubwa na misuli ya katikati inakaribia kuuma ... tafuta tape measure ujaribu ...
Kwa hiyo mara nyingi tunayopimaga 70miguu x 70miguu ni chini ya eka moja, hasa kama miguu haikuwa ya kuruka.
Na ukifanikiwa kum-convince anayekuuzia mkapima eka moja kama 70m x 70m , basi utakuwa umemlalia kiaina kwa sababu 70m x 70m = 4,900 square meters ambayo ni zaidi ya eka moja (4,046.85642 sqr meters). Eneo utakalokuwa umejiongezea laweza kutosha kufugia kuku.
Kama wewe ni mtu wa kununua na kuuza viwanja sana, ningekushauri ununue kifaa cha GPS kinachoweza kukokotoa eneo papo hapo. Unaiwasha tu, unazunguka kiwanja, unabonyeza button, inakupa mita za mraba za eneo, hupunji mtu wala mtu hakupunji.
Kwa mfano Garmin GPS 76 https://buy.garmin.com/shop/shop.do?pID=164#specsTab
Hiyo 30 x 50 haifiki nusu eka, iwe ni miguu au meters.