MKuu Taarifa yako haijitoshelezi!
Kiwanja kipo Mkoa wa Mwanza
Mkoa wa Mwanza wilaya ya..........
Wilaya ya............,Kata ya ............
Mtaa wa ...............
Huduma za kijamii kama;
1.Huduma ya Umeme imefika kiwanja kilipo au bado?
2.Huduma ya maji inapatikana?
3.Vipi kuhusu miundombinu ya Barabara?
4.Vipi mawasiliano ya simu?(Kuna maeneo mengine upatikanaji wa mtandao espeshali internet ni kipengele) Hapo Je Hali ikoje?
5.Eneo ni Kwa ajili ya makazi ya watu?,Isije unakuja kununua eneo ambalo liko kwenye maeneo ya Viwanda,makanisa/misikiti,Starehe (Bars and Lounge) halafu mwisho wa siku ikawa ni kelele mwanzo mwisho!
6.Umbali wa kutoka hapo kilipo kiwanja hadi ilipo Barabara kuu ni kiasi gani?
7.Hapo kilipo kiwanja hadi kufika mjini (Wilayani au Jijini) ni umbali kiasi gani?
8.Eneo lipo Bondeni,Tambarare au mlimani?
9.Eneo ni lako au wewe ni dalali?
10.Je eneo limepimwa tayari Kwa ajili ya makazi na halmashauri ya mji,wilaya au Jiji?,Isije Kuwa eneo lipo barabarani,eneo la wazi,eneo la Jeshi,eneo lililotengwa maalumu na serikali Kwa shughuli maalumu!
Hebu tuondoe Wasiwasi,kama hakuna tatizo nifike na mwanasheria wangu kujipatia hilo eneo!