Nauza mpunga

Nina gunia elfu moja za mpunga.

Zenye ujazo wa debe 7, asilimia kubwa ya mpunga huo ni kalamata.

Bei ya gunia ni laki moja na elfu kumi. (110,000/=)

Eneo ni Tabora mjini.

Namba ya simu. 0686225633
Karibu
Sawa kiongozi tumekupata,naomba kuuliza Gunia moja la mpunga ukikoboa unapata kiasi gani plz naomba kujua
 
Mkuu mpunga mwaka huu hakuna,mvua zimegoma subirsubir upige hela mkuu.
Uko sahihi japo muda mwingine bei kupanda na kushuka huwa Kuna factor nyingine ndogo ndogo. Ila hopefully bei itapanda. Shukrani
 
Mkuu hizo gunia ulinunua ama umezipata kwenye kilimo, na kama ni kilimo ulilima heka ngapi?
 
Mpunga wa kukusanya hauwezi kuwa wote mbegu moja, ndio maana nikawa specific kwamba mwingi ni kalamata, and aina nyingine Kuna beyenge kidogo.

Sijachanganya, ila katika hizo elfu moja kalamata ni zaidi ya 75%
Nyinggi Kalamata, zingine ni mchanganyiko sio?
Za kununua zimetengwa au kuchanganywa , kwa maana ya kupiga bwiwi au chepe?
 
Mali haswa,,, ! Kama ukiweza kuvumilia kidgo utapiga pesa nzuri sana, na utauza kwa kuringa ! Mvua msimu huu sio nyingi,,,wakulima wengi wameangukia masikio ! Kila la kheri ! Natamn siku moja niwe nafanya hii biashara ! Namiliki machine ya kukoboa mpunga, store kubwa ya kukusanyia mpunga kutoka kwa wakulima,,, ! Alafu mchele naupark kwa 5kgs, 10kgs, 25kgs, 50kgs na 100kgs nauza ! Ila kulima hapana, kulima kutegemea mvua ni sawa na kubet ! Kila la kheri ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…