Nauza shamba ekari 50 zote zimepandwa Mananasi

Nauza shamba ekari 50 zote zimepandwa Mananasi

beko

Senior Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
191
Reaction score
92
Kwa yeyote anaehitaji shamba ekari 50 linauzwa, zote zimepandwa Mananasi, kati ya hizo ekari 30 tayari mamanasi yanazaa, na hizo ekari 20 yataanza kuzaa mwakani mwezi December.

Shamba lipo Rufiji, maeneo ya Jaribu. Kila ekari moja ni shs million 5. mazungumzo yapo. Kwa ufafanuzi, ekari moja ina mananasi 3,400. kwa hiyo kwa mwaka kila ekari moja itakupa mapato yasiopungua shs.3,000,000.

Kwa maana hiyo baada ya mwaka mmoja tuu utarudisha takriban 60% ya pesa yako. kwa anaehitaji please send pm
 
Kwa yeyote anaehitaji

shamba ekari 50 linauzwa, zote zimepandwa mananasi, kati ya hizo ekari 30 tayari mamanasi yanazaa, na hizo ekari 20 yataanza kuzaa mwakani mwezi December. shamba lipo Rufiji, maeneo ya Jaribu. Kila ekari moja ni shs million 5. mazungumzo yapo. Kwa ufafanuzi, ekari moja ina mananasi 3,400 . kwa hiyo kwa mwaka kila ekari moja itakupa mapato yasiopungua shs.3,000,000. Kwa maana hiyo baada ya mwaka mmoja tuu utarudisha takriban 60% ya pesa yako. kwa anaehitaji please send pm

Hapo kwenye bold kuna walakini. Ekari moja ya mananasi Kwa uchache inatakiwa iwe na miche isiyopungua 10,000. Wengine wanapanda Hadi miche 24,000.
 
bora ya wewe uliyegundua hilo mana siye wenngine hatuko kwenye kilimo kwanza naona ametuchakachua kiaina best
Hapo kwenye bold kuna walakini. Ekari moja ya mananasi Kwa uchache inatakiwa iwe na miche isiyopungua 10,000. Wengine wanapanda Hadi miche 24,000.
 
ina inawezekana hilo shamba likawa si lake kwani anaonekana ni dalali asiyejua udalali kazi yake
anatoa tangazo roborobo bila kukaizia tangazo lake wateja tufahamu vizuri

hapa best inabidi kuwa makini vinginevyo mtu anaweza kuingiza changa la macho
Yaani best we acha tu jamaa katuchakachua kinoma, teh teh. Tumemstukia huyu
 
Hapo kwenye bold kuna walakini. Ekari moja ya mananasi Kwa uchache inatakiwa iwe na miche isiyopungua 10,000. Wengine wanapanda Hadi miche 24,000.
mi mwenyewe nimeshanga acre inachhukua nanasi 18000-24000. huyu mwenye 3400 itakuwa kama 1/7 ya acre kwa hiyo atakuwa na ekari 50/7=7. huyu bwana anaa ekari saba na anadai 50!!
 
mi mwenyewe nimeshanga acre inachhukua nanasi 18000-24000. huyu mwenye 3400 itakuwa kama 1/7 ya acre kwa hiyo atakuwa na ekari 50/7=7. huyu bwana anaa ekari saba na anadai 50!!

Idadi ya Mananasi kwa kila hekari sio issue sana, pengine ye kayapanda kwa "spacing" kubwa sana hivyo yameingia machache!!
 
kama ni hivyo wauza mananasi wana hela

Mkuu wanaopata pesa nyingi ni hawa wanaokuja kuuza sokoni. Nimeuliza jana nanasi kubwa naambiwa Tshs. 3000 - 5000 wakati shambani wananunua Kwa flat rate ya 1000. Na usafiri si mbali sana kutoka hapo Bagamoyo au Mkuranga kuja Dar. Ila ukiweza kupata wanunuzi hata wa kwenye magenge ukawasambazia Kwa Tshs. 2500 Kwa nanasi, ekari moja unavuna si chini ya milioni 25.
 
Back
Top Bottom