Nauza vifaranga vya kuku aina ya kanga(chotara)

Nauza vifaranga vya kuku aina ya kanga(chotara)

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
26,486
Reaction score
51,156
Habari wanajf?
..karibuni tuendeleze gurudumu la ufugaji,
..kwa anaehitaji vifaranga vya kuku machotara wa nyama na mayai pia, wenye umri wa mwezi mmoja wakiwa tayari wamekwisha chanjwa namkaribisha,
...kwa wahitaji waliopo mikoa ya Arusha,Dodoma,Manyara,Dar-es-salaam,Singida,Tabora pamoja na Shinyanga karibuni PM
 
Weka namba yako tafadhali achana na Waziri Mkuu
 
Ungeweka location uliyopo hizo shm
 
Tuwekee tu bei hadharani wateja Tupo....namba Yako pia
 
wewe haueleweki. unauza kuku au kanga? au wewe una breed mpya ya kuku? kuwa specific na uweke picha ya hivyo vitu unavyouza
 
Nina mashaka na ujasiriamali wako coz hujaweka namba ya simu na bei za hao kuku/kanga. Uko dunia gani? digital au analogia? kwa makini na unachokifanya
 
Mbona umekuwa mkali? nilishataka kuweka toka jana ila huku umeme umekua tatizo
Nina mashaka na ujasiriamali wako coz hujaweka namba ya simu na bei za hao kuku/kanga. Uko dunia gani? digital au analogia? kwa makini na unachokifanya
 
Bei kwa kifaranga ni sh.3500 wanakuziwa singida na unasafirishiwa mpaka mkoa uliopo,(kwa mikoa niliyotaja hapo juu)
 
Tupia picha ya vifaranga na mama zao tuthaminishe mbegu mama tununue!
 
Hauko serious mkuu, mana mambo kama hii watu wanaweka physical adress na namba ta simu.asante kwa kushiriki na wewe humu JF
 
Hiyo ni Biashara tafuta mbinu yoyote uweke picha.nenda internet cafe.
 
Back
Top Bottom