MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Binafsi huwa ninapenda sana simulizi ambazo zina uhalisia wa maisha ya kila siku tunayoishi hususan kwetu sisi wapambanaji na watafutaji wa kila siku. Yaani simulizi ambazo msimuliaji ndiye mhusika na anasimulia kuhusu experience yake katika jambo au mambo fulani sanasana masuala ya utafutaji pesa, utajiri,hustle za maisha aliyoyapitia mpaka kufanikiwa au kufanikisha jambo fulani, ujasusi kidogo sio mbaya n.k Binafsi sivutiwi kabisa na simulizi za mapenzi, au kama zikichomekewa basi zisizidi sana (tatizo siku hizi wasimuliaji wengi wanalazimishia story za mahaba ndani ya simulizi zao) kitu ambacho kinaondoa kabisa uhalisia.
Sivutiwi na simulizi zilizokaa mtindo wa riwaya mfano wa hekaya za abunuasi.Unakuta msimuliaji anasimulia kuhusu maisha ya mtu mwingine! Wakati mwingine majina hayana uhalisia, utasikia mara franfurt, Jean pierre mara safari kuelekea New Orleans! au zile utasikia "Elliot Craig aliruka sarakasi na kumyatulia risasi Brown Carter" Hizo huwa naona zinekaa kitoto na kisekondari sana 😄
Binafsi navutiwa na ninapata mafunzo na hamasa za kimaisha nikisoma simulizi za baadhi ya waandishi humu jf kama UMUGHAKA, Analyse, SteveMollel, (kuna ile simulizi moja ya "Laana za maiti") mwandishi simkumbuki, Na simulizi zingine kama Magofu ya Rhapta (japo mwandishi alianza kuingiza mapenzi) n.k Kuna moja nimesoma juzi kati japo ameishia njiani (kutoka kwenye utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!)
by Poker n.k n.k
Sasa naendelea na msako kutafuta simulizi zingine za aina hii 😎