Ballerina
JF-Expert Member
- Jun 2, 2011
- 386
- 187
Hahah..eketerewa kila siku mleu...ngameny kapisa!!!
Yeesu lanye.......kulakoye naore mbaka.....?Mbie auye mndenyi ko wameku,wamrundie kindo..................tukeri pamojaa.........?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahah..eketerewa kila siku mleu...ngameny kapisa!!!
aore mbakafo..nyi mndu mcha kapisa!
kitewo nkiki ulemo mangi?! ayang, ngakutirimia....
mh pole kaka
njoo kwangu ntakupenda
dahh pole mshkaji...bt jchek unakosea wap..uenda unakosea somewhre bila kujijua ..ata km unaprovide vyooooooooote bt kuna vtu tunaviitaji...ebu jchek fresh..uenda unakosea sehemu....
najua ni wewe si kaka yako wala nani.....:A S-baby:
ok..wakubwa wanaogopa kumwuliza asijekurupuka kuingia kwenye ndoa...kisa walim-pressure sana!
Kuna wakati mama alimuuliza sana, mpaka yeye mwenyewe mama akajishtukia (only that she didnt know the truth!)..so, now wanaogopa kumuliza sana asije ona wanamlazimisha...!
wewe huwezi kumsaidia!??[/QUOT
Hakuwahi kupiga mechi za mchangani huyo? Aache undondocha nae...Asaidiwe nini sasa Kupanua mapaja au? eti mama anaogopa..Huyo ni Mwanaume au Wa KIUME?
Habari zenu wandugu,
Ni mkasa ulomtokea kaka yangu. Japo nimeuweka in poem form, I hope haujapoteza maana. I hope kuna jambo tutalojifunza..Its areal life story, he is 34yrs now na bado hajaoa. Nimekuwa nikimsumbua kwa maswali ila juzi kaamua kunipasulia ukweli...Ingekua wewe, ungeendelea kupenda kweli!???
Machungu na simanzi, tele vimejaza moyo
nishajifunga kitanzi, sitaki kutiwa moyo
silitaki tena penzi, limenipondea moyo
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Penzi silitaki tena, moyo limenipondea
nilimpenda Irena, ngoma nilimchezea
hakuhitaji kunena, vyote nilimletea
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Minne nayo miaka, meno akanichekea
kajua mwisho wa mwaka, ndoa tutajifungia
kawajua zangu kaka, wazazi na dada pia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Siku moja nimelala, simu nikaipokea
anajiita Matumla, tena akanifokea
mkewe niache mla, ndumba angenitumia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Sa mi ningejuaje, Irena ameolewa
tumesoma wote nje, -kumbe- nyumbani anangojewa
linipoza wananjenje, na nyimbo nikatungiwa
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Miezi tisa kapita, na moyo nimeufunga
nikamuona Anita, upole ndo ulonifunga
kasahau yalopita, safari tukaifunga
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Mpole, mzuri sura, mcheshi nakuambia
kasoma Makutopora, mjeshi alotimia
n'kaapa h'watonipora, moyoni keshaingia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Siku kuzaliwa kwake, keki nikamletea
kamlisha wangu mke, kisha kanitapikia
kamkimbiza Temeke, -ati- aleji memzidia
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Hongera nikapokea, ati ya miezi sita
kashindwa hata kulia, moyo kwenda ukasita
tulingoja hadi ndoa, vipi mama hukuniita
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.
Mengi mekutana nayo, Ana, Linda na Jesicca,
wamenichezea moyo, sitaki tena ushika
kitanzi nimeufunga, kupenda mpende nyie
nawaachia malenga, hukumu wanitajie.