Cowman
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 1,715
- 3,158
Majira yame badilika usikubali kuwa na biashara moja mjini ,Fanya kilimo,ufugaji,uwekezaji na biashara zote za fani yako Pamoja na Elimu yako bila hivyo utaishia kuona mafanikio kwa wezio na tambua hakuna mchawi wa mafanikio yako tofauti na uoga wako.
Usiogope kufeli, jifunze kufanya utafiti wa kina kabla hujaanza chochote cha kukuingizia Pesa,watambue wateja wako na mahitaji yao kwanza Pesa zitakufuata...usiende kwa mganga maana nae pia anatafuta Pesa, Hakuna mwanadamu anaeweza kukupa furaha ya mafanikio maana tume umbiwa uchoyo. Usimtegemee Mwanadamu mwenzio ila Mungu Pekee.
Weka mipango yako pale unapokuwa huna chochote ndipo Mawazo huwa yanakuja, yaandike sehemu salama na uyafanyie kazi moja baada ya jingine kwa kipaumbele cha kutegemeana. Biashara ziendane na zitegemeane na wakati mwingine zisiwe na uhusiano kabisa."Usiweke mayai yote kwenye kapu moja" Wallen Buffet.
Hata kama upo kwenye ajira,Fanya zaidi ya ajira ebu fikiria,ule muda wa jioni huwa unaufanyia nini? Tuwe na ratiba binafsi na tuifuate kwa uaminifu na Mungu atatubariki katika hayo. Tenga muda wa mapumziko ya mchana yasiyo zidi nusu SAA na Siku maalumu ya Ibada na isihusiane na Biashara bali na ukaribu na familia Pamoja na marafiki.
Kumbuka kuwa tembelea,Wafungwa magelezani,Yatima na watoto wanao ishi katika mazingira magumu Pamoja na wagonjwa walioko mahospitalini...utaona jinsi Mungu alivyo kubariki kwa afya na uzima, tabia hii itakufundisha kushukuru na ndio mfumo pekee wa kutoa Sadaka unaokubalika hata Mbinguni.
Penda familia yaani Ndugu,Watoto,Mkeo/Mmeo,majirani,Marafiki na washiliki wa imani moja na shiriki nao katika Furaha na huzuni katika wakati husika,Muda wako Pamoja nao wakati huo huwa wa thamani kuliko fedha na Mali zako.
Usingojee kuajiriliwa au kufikia mtaji Fulani ndipo uanze biashara uipendayo kama njia mbadala wa kukupatia Pesa,weka Malengo na hakikisha hakuna binadamu anayaingilia.Wengi wamekuwa masikini kwa kusikiliza maoni ya Wazazi,Ndugu,Mchungaji na Mwalimu ila sio msukumo ulioko mioyoni mwao.Mafanikio hayana umri endelea kupambana hadi kieleweke.Tarehe hazirudi nyuma na Siku hazigandi ifanye Jana isiwe bora kuliko Leo.