Nawaandikia Vijana Wenzangu Kwa Kuwa Nina Imani Mna Nguvu Ndani Yenu.

Nawaandikia Vijana Wenzangu Kwa Kuwa Nina Imani Mna Nguvu Ndani Yenu.

Cowman

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
1,715
Reaction score
3,158
Majira yame badilika usikubali kuwa na biashara moja mjini ,Fanya kilimo,ufugaji,uwekezaji na biashara zote za fani yako Pamoja na Elimu yako bila hivyo utaishia kuona mafanikio kwa wezio na tambua hakuna mchawi wa mafanikio yako tofauti na uoga wako.

Usiogope kufeli, jifunze kufanya utafiti wa kina kabla hujaanza chochote cha kukuingizia Pesa,watambue wateja wako na mahitaji yao kwanza Pesa zitakufuata...usiende kwa mganga maana nae pia anatafuta Pesa, Hakuna mwanadamu anaeweza kukupa furaha ya mafanikio maana tume umbiwa uchoyo. Usimtegemee Mwanadamu mwenzio ila Mungu Pekee.

Weka mipango yako pale unapokuwa huna chochote ndipo Mawazo huwa yanakuja, yaandike sehemu salama na uyafanyie kazi moja baada ya jingine kwa kipaumbele cha kutegemeana. Biashara ziendane na zitegemeane na wakati mwingine zisiwe na uhusiano kabisa."Usiweke mayai yote kwenye kapu moja" Wallen Buffet.

Hata kama upo kwenye ajira,Fanya zaidi ya ajira ebu fikiria,ule muda wa jioni huwa unaufanyia nini? Tuwe na ratiba binafsi na tuifuate kwa uaminifu na Mungu atatubariki katika hayo. Tenga muda wa mapumziko ya mchana yasiyo zidi nusu SAA na Siku maalumu ya Ibada na isihusiane na Biashara bali na ukaribu na familia Pamoja na marafiki.

Kumbuka kuwa tembelea,Wafungwa magelezani,Yatima na watoto wanao ishi katika mazingira magumu Pamoja na wagonjwa walioko mahospitalini...utaona jinsi Mungu alivyo kubariki kwa afya na uzima, tabia hii itakufundisha kushukuru na ndio mfumo pekee wa kutoa Sadaka unaokubalika hata Mbinguni.

Penda familia yaani Ndugu,Watoto,Mkeo/Mmeo,majirani,Marafiki na washiliki wa imani moja na shiriki nao katika Furaha na huzuni katika wakati husika,Muda wako Pamoja nao wakati huo huwa wa thamani kuliko fedha na Mali zako.

Usingojee kuajiriliwa au kufikia mtaji Fulani ndipo uanze biashara uipendayo kama njia mbadala wa kukupatia Pesa,weka Malengo na hakikisha hakuna binadamu anayaingilia.Wengi wamekuwa masikini kwa kusikiliza maoni ya Wazazi,Ndugu,Mchungaji na Mwalimu ila sio msukumo ulioko mioyoni mwao.Mafanikio hayana umri endelea kupambana hadi kieleweke.Tarehe hazirudi nyuma na Siku hazigandi ifanye Jana isiwe bora kuliko Leo.
 
Safi sana" .. bandiko safi maarifa pevu ".. ila hapo kuacha kwenda kwa waganga sinto patilia maanani aisee"... kwa sababu sio mganga tu anayezisubiri pesa zetu" Hata misikiti na makanisa inazitaka pesa zetu ili yaweze kujiendesha "...
 
Msikitini na Kanisani wanasali watu, zinahitajika pesa kwa ajili ya kuendesha IBADA na mambo mengine. Mchungaji anayetaka kutajirika kupitia SADAKA zetu haendi mbinguni.
 
Asante sana mkuu kwa bandiko murua....ila ktk maisha hakuna kitu kizur kama kufanya kitu kikupacho amani ya moyo ...na kingine pia kujielewa unataka nini maishani ni jambo zuri sana...
Naongea HV kwa sababu baadhi ya watu wamejikuta wakifanya mambo wasiyoyafurahia kisa tu wamehamasishwa na watu wengine....mfano kuna baadhi ya watu hawapendi kufanya biashara kabisa no matter what they gain,wao furaha yao ni kuhudumia jamii kwa kile kinachowapa furaha,maybe MTU n daktari na hii unakuta n kazi ya ndoto yake na hajawah dream kabisa kufanya biashara na pengine hainjoi kufanya biashara kabisa...so all in all doing what u love and what gives u a peace of mind and heart is worthfull than doing a more paying project which doesn't make u happy....
MTU afanye vtu vinavyomfanya yeye aishi maisha ya furaha zaidi,furaha n muhimu zaid
 
Ni kweli mkuu si kila mtu anaweza kufanya biashara, ukifanya unachokipenda utaenjoy na utakuwa na amani sana. Lakini pia unaweza kufanya biashara ya fani au elimu yako si kila mtu afungue duka kariakoo.
 
Usikope kuanzisha biashara mkuu, utafeli TENAAA!
Unajua nn chief mawazo hayo kama mmi yapo kichwani kwa muda mrefu sana na,natumikia deni adi sasa april namaliza,

Ni mtumishi wa chini kabisa, mshahara usiozid lak tatu,sasa nawezaje kufanya haya kwrnye hui uzii,
Nawaza kwenda shule ili niboreshe mshahara.lkn bado mambo yamegandaaaa
NIMEDUWAAA
 
Be strong mkuu naamini bado hujachelewa, ukimaliza mkopo anza kusave kidogo kidogo after months utakuwa umejaza kibaba. Wazo za kurudi shule si baya pia!
 
Back
Top Bottom