LOL...'Sipiyu' wewe ni mchokozi sana aisee, khaaa? ...ha ha ha!
Mkuu wangu Moskwito
Mimi namheshimu sana huyu mdada, namjali na nampenda pia
Na naonyesha hayo kwa VITENDO
Wanasema "KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA"
Hasira si nzuri kabisa, hasa hasira za kuzidi ambazo unaweza kuzihamishia kwa mtu mwingine pia
Bila kujali sababu zake, HASIRA SI NZURI HATA.
I may sound like mchokozi, mkorofi lakin tafakari kwa makini maneno yangu
Wakati wewe umempa ushauri mzuri sana wa kushusha hasira zake, mimi nimemueleza namna hasira zinavyoweza kuharibu zaidi badala ya kujenga. Na anapaswa kuepuka hasira za kumfanya mpaka anajiapiza, hasa anaposema ". . . . kuanzia leo"
Tubembelezane kushusha hasira lakin TUJENGANE PIA kuepuka kutawaliwa na hizi hasira.
Anaweza kujidhuru hata kiafya kwa kufanya hivi
Wanasema "KINGA NI BORA KULIKO TIBA"
Kila binadamu ana hasira, lakin hebu fikiria kila mtu angekuwa hawezi kudhibiti hasira zake . . . .
Tufarijiane na tufundishane pia
Tusioneane aibu wala woga Mkuu
Nadhani unanielewa ninachomaanisha